ASILI YA DHAMBI, JE UBATIZO NI LAZIMA?



ASILI YA DHAMBI
Inabidi kusisitiza kwamba dhambi hutoka ndani yetu. Ni kosa letu hata kutenda dhambi. Bila shaka, ingekuwa vema kuamini kuwa halikuwa kosa letu hata tukitenda dhambi. kwa hiyari tungetenda dhambi na halafu kutoa udhuru wenyewe kwa kuwaza kwamba kweli lilikuwa kosa la Ibilisi na ya kuwa lawama kwa dhambi yetu ingewekwa kabisa juu yake. 

Sio ajabu sana kwamba katika kesi ya mwenendo mbaya sana, mtu mwenye kosa anaomba msamaha kwa kuwa anasema ya kwamba alishikwa na shetani kwa muda na kwa sababu hii yeye mwenyewe hahusiki. Lakini ni sawa kabisa, udhuru huu dhaifu unahukumiwa kwa sababu hauna msingi kabisa, na mtu anapotishiwa hukumu juu yake.

Tukumbuke kuwa "mshahara wa dhambi ni mauti" (Rum. 6:23); dhambi huleta kifo. Kama sio kosa letu kutenda dhambi, bali ni Ibilisi, Bali Mungu mwenye haki yampasa amwadhibu Ibilisi kuliko sisi. Lakini ukweli ni kwamba tunahukumiwa kwa ajili ya dhambi zetu wenyewe yaonyesha tunahusika kwa dhambi zetu. 

Wazo la kwamba Ibilisi ni mtu dhahiri aliye nje yetu kuliko kwamba ni jambo la dhambi ndani yetu ni kujaribu kuondoa kuhusika kwa ajili ya dhambi zetu. Lakini huu ni mfano mwingine watu wanapokataa kupatana na Biblia inapofundisha kuhusu mwili wa binadamu: huo kwa asili ni wenye dhambi.

"Hakuna kitu kilicho nje ya mtu ambacho kikimwingia chaweza kumtia unajisi ….. Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, Uasherati, wivu, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya ….. kiburi, upumbavu: haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi"(Marko. 7: 15 -23).

Wazo la kwamba kipo kitu fulani nje yetu kinachotuingia na kutusababisha kufanya dhambi halilingani na mafundisho yaliyo wazi ya Yesu hapa. Toka ndani, ya moyo wa mtu, hutoka yote haya mambo mabaya. Hii ndiyo sababu wakati wa gharika, Mungu aliona kwamba "mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake"(Mwa. 8:21. Yak. 1:14) anatuambia namna tunavyojaribiwa:"Kila mmoja (yaani mwanadamu) hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa" Tunajaribiwa kwa tamaa zetu wenyewe, mawazo yetu mabaya; sio kitu kingine chochote nje yetu. "Vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyo kati yenu" ?.

 Yakobo anauliza; "Si humu katika tamaa zenu ?" (Yak. 4:1). Kila mmoja wetu ana majaribu yake binafsi. yanazalishwa na nia zetu mbaya, kwa sababu ni yetu wenyewe. ukweli umesemwa ya kwamba sisi wenyewe ndio adui zaidi mbaya.

Kitabu cha Warumi kwa upana kinahusika na dhambi, asili yake, na jinsi ya kuishinda. Ni muhimu sana kwamba Ibilisi na shetani hawapatikani sehemu walipotajwa katika kitabu hiki; kwa maneno ya kusema kuhusu asili ya dhambi, Paulo hamtaji Ibilisi au shetani. Kwa njia hiyo hiyo'Ibilisi’ ni dhana ya Agano Jipya. 

Kama yupo kiumbe aliye nje anayefanya tutende dhambi, kwa kweli asingetajwa kwa upana katika Agano la Kale ?. Bali upo ukimya wa maana uliokwenda chini kuhusu hili. Taarifa ya kipindi cha waamuzi au Israeli jangwani, zinaonyesha ya kwamba nyakati hizo Israeli walitenda dhambi sana. Lakini Mungu hakuwaonya kuhusu kiumbe mwenye nguvu kuwa atawaingia na kuwafanya watende dhambi. Badala yake, aliwasisitiza kushika neno lake, ili wasivutwe kwenda nje ya mapenzi yake na kuufuata mwili wao (K/Torati 27:9,10; Yoshua 22:5)

Paulo analia:"Ndani ya mwili wangu halikai neno jema …. Kutenda lililo jema sipati ….. Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ile dhambi ikaayo ndani yangu"(Rum. 7:18 -21). Kutenda kwake dhambi hamlaumu kiumbe aliye nje aitwaye Ibilisi. Anaweka kwenye mwili wake mbaya kuwa ndiko asili ya dhambi:"Sio mimi nafsi yangu, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu". 

Basi, nimeona sheria hii (ndani yangu), ya kuwa kwangu mimi nitakaye kutenda lililojema, lipo lililo baya (yaani - ndani) yangu. Hivyo anasema kwamba kipingamizi cha kuwa kiroho kinatoka kwingine anapoita"dhambi ikaayo ndani yangu". kila mtu mwenye mawazo ya kunia kiroho atafikia kwenye mawazo hayo hayo. Ijulikane ya kwamba hata mkristo mkubwa kama Paulo hakuona badiliko la mwili baada ya kuongoka, wala hakuwekwa kwenye nafasi ambayo hawezi kufanya dhambi. 

Makundi ya siku hizi ya "Kiinjili" yanadai kwamba wapo katika nafasi hii ya kutotenda dhambi, kwa hivyo wanamweka Paulo vema ndani ya 'wasiookoka’ kwa sababu ya taarifa yake hapa katika Rum. 7: 15 -21. Mistari hii imewaletea shida kubwa kwa madai yao. Daudi, mwingine pasiposhaka mtu mwenye haki, vivyo hivyo alifafanua juu ya mwili wake kabisa mwelekeo wa daima wa dhambi: "Tazama mimi naliumbwa katika hali ya uovu, mama yangu alichukuwa mimba hatiani - dhambini"(Zab. 51:5).

Biblia ipo wazi kabisa kuhusu ukubwa na ubaya wa mwili wa binadamu. Kama hili likikubalika, hakuna haja ya kutafuta mtu wa kufikiriwa aliye nje ya mwanadamu anayehusika na dhambi zetu. Yer. 17: 9 unasema kwamba moyo wa binadamu huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote ambapo hauwezi hasa kukubali upana mbaya sana wa dhambi zake. 

Naye Yesu alitia alama pia mwili wa mwanadamu kwa asili ni mbaya katika Math. 7:11; Mhubiri 9:3 (andiko la Kiebrania) halikuweza kuwa wazi;"Moyo wa wanadamu umejaa uovu", Efe. 4:18 inatoa sababu ya mtu asili ya kutengwa toka kwa Mungu kuwa ni "kwa sababu ya ujinga uliomo ndani yao, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao". Ni kwa sababu ya upofu wa kiroho na ujinga wa mioyo, njia zetu za kufikiri zilizo ndani yetu, ndizo zimetuweka mbali na Mungu. 

Pamoja na mstari huu, Gal. 5:19 unasema dhambi zetu kuwa ni"Matendo ya mwili"; ni mwili wetu wenyewe, utu wetu kabisa na umbo, ndivyo hutufanya tutende dhambi. Hakuna hata fungu la maneno linaloeleza asili ya dhambi ndani yetu kuwa zimekuwemo kwa sababu ya Ibilisi aliyeziweka; maelekeo ya dhambi ni mambo mengine ambayo kwa kawaida tunayo tangu kuzaliwa; ni sehemu kubwa ya umbo la mwanadamu.



Post a Comment

0 Comments