ASKOFU MWENYE WATOTO 10 AOA MKE MWINGINE, BAADA YA TALAKA

Askofu Mkuu wa Kanisa la Furaha hapa nchini (KLFT) Jones Molla ameoa mwanamke mwingine baada ya mahakama kutoa talaka ya ndoa yake ya kwanza waliyofunga mwaka 1978 baina yake na Lilian Kimambo.
 ASKOFU MOLLA AKIONYESHA PETE YA NDOA MUDA MCHACHE KABLA YA NDOA HIYO KUFUNGWA KATIKA KANISA LA BIBILIA MJINI MOSHI (Picha na Jabir Johnson).

Tukio hilo limefanyika Jumapili ya Desemba 21 mwaka huu. Itakumbwa kwamba, Mahakama ya Mwanzo mjini Moshi mkoani hapa ilitoa hukumu hiyo katikati ya mwaka huu ikivunja rasmi uhusiano huo. Mke huyo wa kwanza walizaa naye watoto 10 na sasa ana wajukuu kadhaa.
Shughuli za kufunga harusi na mke huyu wa sasa zimefanyika katika Kanisa la Biblia, lililopo maeneo ya Pasua - Boma Mbuzi.

Hebu tazama picha hizi.













  ASKOFU MOLLA AKIMBEBA MKEWE BAADA YA NDOA HIYO KUFUNGWA KATIKA KANISA LA BIBILIA MJINI MOSHI (Picha na Jabir Johnson).

CHANZO: JAIZMELALEO

Post a Comment

0 Comments