Kitabu cha Mwanzo katika Biblia




Kitabu cha Mwanzo (pia: Kitabu cha kwanza cha Musa; kwa Kilatini Genesis) ni kitabu cha kwanza katika Biblia

Kwa asili kimeandikwa kwa Kiebrania, na katika lugha hiyo kinaitwa בְּרֵאשִׁית, Bereshit, ambalo ni neno lake la kwanza, lenye maana ya “mwanzoni”.

Pia ni kitabu cha kwanza cha Torati (au: Torah, maana yake sheria ya kidini ya Wayahudi), yaani vitabu vitano vya kwanza vya Agano la Kale (kwa Kigiriki Pentateuko). Wengine wanaviita vitabu vitano vya Musa kwa vile inafikiriwa kuwa ndiye mwandishi wa vitabu hivyo.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.
Katika kitabu hicho kimeelezea mwanzo wa kila kitu.

Maana ya kitabu cha Mwanzo ni 'Asili', na jina hili linafaa kwa kitabu cha Biblia kinachosimulia habari za asili ya ulimwengu, ya binadamu, ya dhambi zao na njia ya Mungu ya kuwaokoa.

Kitabu cha Mwanzo kina sura hamsini. Katika sura 1 hadi 11, historia ya awali juu ya binadamu inasimuliwa. Sura 12 hadi 50 inahusu historia ya kale ya Waisraeli. Hasa zinataja hadithi juu ya wazee au mababu wao, kama Abrahamu, Isaka, Yakobo na Yosefu.









Post a Comment

0 Comments