Maisha ya Ayubu yalibadilika kabisa; Kwanza alipoteza mali zake zote. Pili,watoto wake walikufa. Tatu alikuwa mgonjwa sana. Yote hayo yametokeaghafla.
Akiwa amekata tamaa, Ayubu alisema; “Nafsi yangu inachoka na maisha yangu; Sitajizuia na kuugua kwangu; Nitanena kwa uchungu wa roho yangu; (Ayubu 10:1)Akaongeza kusema; “Mimi nikiwa mbaya, ole wangu…Mimi nimejaa aibu; Nakuyaangaliwa mateso.” Ayubu:10:15
Hata hivyo ijapokuwa alikuwa katika dhiki; Ayubu hakumwacha Muumbawake. “Je, tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya? Katikamambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi kwa midomo yake.” Ayubu 2:10
Mabadiliko maishani mwake hayakumbadili. Hivyo Ayubu ni mfano mzuri wauvumilivu.Unapokumbwa na matatizo huenda wewe pia ukachukizwa na uhai wako.Hata hivyo kama Ayubu, unaweza kuwa mtu asiyebadilika hata maishayakibadilika Yakobo 5:11.
Kama Mungu alimjali Ayubu, naye anakujali nawewe!
Ayubu ni mfano wa kuigwa; anaandika
Anko Tununu
17 Februari 2026
mcrctv@gmail.com
