Dibaji ya Waliotafsiri Biblia kwa Wasomaji



Hii ndiyo tafsiri mpya ya Neno la Mungu katika lugha ya Kiswahili, nayo
imefanywa kwa matumizi ya Wakristo wa Kanisa la Mungu katika nchi zote
kunakosemwa Kiswahili. Tafsiri nyingi za Kiswahili zilizo mbalimbali zimefanywa
siku zilizopita, za Agano la Kale, na za Agano Jipya. Tunawashukuru sana watu
hao waliofanya tafsiri hizi tunazozipenda, ambazo kwa hizo tumepata baraka kuu
za kirohoni.

Lakini haiwezekani kwamba watu wa British and Foreign Bible Society, huko
London, waendelee kupiga chapa Biblia katika msemo wa Kiswahili cha Kimvita na
cha Kiunguja, na Societies nyinginezo kupiga chapa tafsiri nyingine nyingine: basi
imedhaniwa na kwamba roho ya umoja itazidi kuonekana katika Kanisa la Mungu
kila mahali katika Afrika ya Mashariki kama ikiwezekana sote tuwe na namna
moja ya Biblia katika Kiswahili. Basi tafsiri hii ilipoanza kutengenezwa ilitupasa
kuchagua na kuyatumia yote yaliyokuwa mema zaidi katika tafsiri za zamani, ili
kufanya kitabu kimoja kipya. Kazi hii imeendelea sasa kwa miaka mingi, na hao
wenye kutafsiri wamesaidiwa katika kazi yao na watenda-kazi wenzi wao wengi,
Wazungu kwa Waafrika, pande zote za Afrika ya Mashariki. Zaidi ya yote tumejua
ya kwamba Mungu Roho Mtakatifu ametuongoza na kutusaidia katika kazi hili
nasi twatumaini sana ya kwamba, kwa nguvu za Roho yeye yule, tafsiri hii nayo
itawaletea baraka kuu wote waisomao.

Hapana budi wasomaji wengine wataona ya kwamba kuna mageuzi ambayo
kwanza hawatayapenda; hili ni lazima kwa Wakristo wa kila mahali, ambao
wamezoea vitabu vyao vya zamani. Pamoja na hayo, pengine maneno hayo
watakayoyakataa watu wasemao Kimvita siyo yale watakayoyakataa wanaotumia
Kiunguja. Basi, na tukumbuke sote kila tutakapokisoma kitabu hiki, ya kwamba
wenye kufanya kazi hiyo wamejaribu sana kutafsiri Neno la Mungu katika lugha
itakayowaelea wote. Wala isidhaniwe kabisa kwamba katika tafsiri hii kuna
mageuzi yo yote yaliyofanywa ya Neno la Mungu. Hasha! jambo hilo haliwezekani
kabisa. 

Lakini, na tukumbuke ya kwamba Neno la Mungu halikuandikwa kwanza
kwa lugha ya Kiingereza, wala ya Kiswahili. Roho Mtakatifu aliwavuvia watu
watakatifu wa kale, Wayahudi na Wakristo, ili kudhihirisha na kutangaza Neno
la Mungu. Hao Wayahudi wakatuandikia Neno hilo kwa lugha ya Kiebrania, katika
Agano la Kale, tena hao Wakristo wakaliandika kwa Kiyunani, katika Agano Jipya.
Basi watu wanaotafsiri Biblia katika lugha za sasa, kwanza huangalia kwa kutunza
sana maneno hayo ya asili yaliyoandikwa zamani katika lugha ya Kiebrania na
Kiyunani; kisha wakajaribu kuandika tafsiri iliyo halisi. Mara kwa mara inawe-
zekana kutengeza kidogo hizo tafsiri zilizotangulia kufasiriwa, nasi tumejaribu
kufanya hivi, pamoja na kuungamanisha hizo tafsiri za kale.

Hiyo kazi yenyewe haikuwa rahisi. Matumizi mbalimbali yametokea katika
janibu mbalimbali za nchi hii. Kwa mfano, ilikuwa hapana budi kufikiri kwamba
hilo Jina la Mungu katika Agano la Kale litaandikwa "JEHOVA Mwenyezi
Mungu'", au "BWANA Mungu". Litakapopigwa chapa kitabu cha Agano la Kale,
kutakuwa na maelezo maalumu juu ya neno hilo. Pia maendelezo ya majina yote
ya watu, na ya mahali, ilikuwa lazima yafikiriwe tena na mengine kutengenezwa;
jambo hili lilikuwa kazi kubwa sana, kwa sababu yako majina zaidi ya 3,500. Tena


jina la kitabu chenyewe lilifikiriwa, kama kiitwe "Maagano Mapya" au Agano
sehemu nyingine za nchi hii, ambayo katika janibu nyingine hutumiwa au kutamkWa
Jipya". Kisha kuna maneno mengi yanayojulikana sana, ambayo hutumika katika sehemu nyingine za nchi hii, ambayo kwa janibu nyingine hutumiwa au kutamkwa vingine. Maneno kama hayo ni mengi kwa mfano "ndege" au " nyuni", "jimbi" au "jogoo" au
"kongwa" au "nira", "nuru" kifudifudi" au kifulifuli". Kila ilipowezekana tumetumia maneno au maendelezyote mawili, mahali mbalimbali. Lakini mara kwa mara imeonekana vema kutumia neno moja, au maendelezo mamoja tu, kama katika maneno haya "telemka" (teremka), "uongo"" (uwongo), "'kinywa" (kanwa),
hatia" (khatiya), "uhai" (uhayi), Pengine kulikuwa na mapatano
sababu neno lenyewe huwa limekwisha kufikiriwa na
yataonekana mwisho wa kitabu hiki.

kuwa neno lililokwisha kufikiriwa na Inter-territorial Committee; bali katika maneno mengine iliwapasa wazee wa Bible Conference au hao wenye kutasiri, kukata mashauri wenyewe. Hivi, "yake" (yakwe) huonekana "kwa kuwa" yataonekana yote mahali mbalimbali; pia "kesho yake" na "siku pili yake", yote mawili yametumiwa. Maneno mengine yajulikanayo sana kama "ili kwamba", na hao watu" katika Kimvita, na "nawaambieni' katika Kiunguja hayatumiwi sana katika tafsiri hii mpya, kwa sababu ni maneno yasiyojulikana sana isipokuwakatika nchi zao.  Tuseme hivi, neno linalojulikana sana ndilo lazima kuleta maana halisi ya neno fulani, basi, panapotukia neno lisilojulikana kwa wasomaji ko kote kunakotumiwa Kiswahili, maelezo ya maneno kama hayo yataonekana mwishoni mwa kitabu hiki.

Liko neno moja ambalo linahitajia maelezo maalumu. Wasomaji waliozoea
kitabu cha Maagano Mapya cha Kımvita wataona neno hili "Amin" limetumiwa badala ya Ni kweli" katika mwanzo wa maneno mengine ya Bwana wetu

"Amin" ni neno lililotumiwa kwanza na Wayahudi mwisho wa sala na mu
Bwana wetu Yesu
wa habari (tazama Hesabu 5:22; Kumbukumbu la Torati 27: 51; 1 Mambo
ya Nyakati 16 :36; Zaburi 41 : 13, na kadhalika).

Kristo alitamka mara nyingi “Amin", katika hiyo lugha ya Kiaramu aliyoitumia
yeye, katika mwanzo wa maneno, ili apate kuonyesha wazi ya kwamba hayo
atakayo kuyasema ni kweli tupu. Tafadhalini mkumbuke kwamba maelfu
Wakristo Waafrika katika nchi mbalimbali wamejua tangu hapo matumizi ya neno
hili Amin", kwa sababu limetumiwa kwa miaka mingi katika tafsiri ile ya Kiunguja

Twawasihi mtuombee sisi tulioshirikiana katika kazi hii, ambao tu wengi
sana, ili kwamba Mungu atubarikie sisi na hayo matunda ya kazi yetu. Sisi nasi
twawaombea ninyi mtakaokisoma kitabu hiki, kwamba baraka ya Mungu ikae
kwenu daima. Na mwisho, ombeni kwa bidii ili kwamba Mungu Roho Mtakatifu
aliyewavuvia hao waandishi wa zamani wa Kitabu hiki amulike pia katika mioyo
ya wote wasomao, na kukitumia siku hizi zetu, ili kuuendeleza Utukufu wake na
kulijenga Kanisa la Yesu Kristo.

Ni sisi
WENYE KUTAFSIRI. 

Previous Post Next Post