Matthew Sasali: Nalikuwa katikati ya Usingizi, Sauti ikaja na kusema, andika.


MCRCTV katika kupitia kurasa mbalimbali katika mitandao ulimwenguni ikakutana na ujumbe huu ambao Mchungaji Matthew Sasali aliuandika katika ukurasa wa Facebook Septemba 26, 2019. Endelea kuusoma na ubarikiwe na Bwana Yesu.

"Pamoja na "UBINADAMU" ulionao...watu wanakuheshimu, wanakusikiliza, wanafuata maelekezo yako, wanakuamini na zaidi wanakueleza na "taabu"zao...

Wewe sasa usijivishe UUNGU, ati kwa Cheo chako ama jina lako basi wewe hukosei, unajua yote, wengine woote wajinga, bila wewe hawatoboi...HAPANA

Hebu nyenyekea, acha kujivuna...hawa WATU ni wa-Mungu na anaweza tu KUWAONDOA kwako na maisha yao yakaendelea ama akaondoa tu KIBALI chake juu yako...ukabaki mtupu, unajisemesha wanakuangalia tu.

Hebu tujifunze kuwaheshimu watu na kuwatumikia!

ZAIDI sana heshimu NAFASI aliyokupa MUNGU maana yeyote anaweza kupewa!!.."

Imetayarishwa na Jabir Johnson…..Oktoba 6, 2019.


Post a Comment

0 Comments