Mchungaji Matthew Sasali ni nani?


Matthew Sasali hupendelea kutumia kauli mbiu ya ‘Mume wa Mke mmoja, Baba wa watoto wanne na Mchungaji wa Wengi’ kwa kiingereza ni ‘Husband of One...Father of Four...Pastor of many’. 

Alizaliwa katika mji wa pwani ya Ziwa Nyasa wa Mbamba Bay, katika miongoni mwa mikoa ya Tanzania wa Ruvuma. Amepita shule mbalimbali katika kuchukua masomo yake Makongo (Dar es Salaam), Milambo (Tabora), pia amesoma Global University. 

Katika masomo ya uandishi wa habari alipata cheti chake Mbeya Institute of Journalism (MIJO), mnamo mwaka 2011 wakati huo alikuwa Meneja wa Redio Ushindi (inamilikiwa na kanisa la Tanzania Assemblies of God) wadhifa aliodumu nao hadi mwaka 2015. 

Aliondoka Ushindi FM kwa ajili ya kwenda masomo nchini Marekani ambako alichukua shahada ya uzamili ambayo alihitimu mwaka 2018. Kwa sasa ni mchungaji wa Kanisa la Calvary Revival  lililop Edmonton nchini Canada tangu mwaka 2017. 

Utume katika uchungaji wa madhehebu ya Kipentekoste alianza muda mrefu. Mnamo Oktoba 2004 alianza kuongoza Kanisa moja mkoani Morogoro, maeneo ya Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine. 

Hapo ilikuwa ni mara baada ya kuhitimu masomo yake katika Chuo cha Biblia na kupata shahada ya kwanza. 

Alichunga kanisa hadi mwaka 2011 alipopewa nafasi ya kuongoza redio kama Meneja.

Post a Comment

0 Comments