Kitabu
cha Mwanzo (pia: Kitabu
cha kwanza cha Musa; kwa Kilatini Genesis) ni kitabu cha kwanza katika Biblia.
Kwa
asili kimeandikwa kwa Kiebrania, na katika lugha hiyo kinaitwa בְּרֵאשִׁית, Bereshit, ambalo ni neno lake la
kwanza, lenye maana ya “mwanzoni”.
Pia
ni kitabu cha kwanza cha Torati (au: Torah, maana yake sheria ya
kidini ya Wayahudi),
yaani vitabu vitano vya kwanza vya Agano la Kale
(kwa Kigiriki
Pentateuko).
Wengine wanaviita vitabu vitano vya Musa kwa vile inafikiriwa kuwa ndiye mwandishi wa vitabu
hivyo.
Kama
vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya
maendeleo ya ufunuo
wa Mungu
kwa binadamu.
Katika kitabu hicho kimeelezea
mwanzo wa kila kitu.
Kitabu cha Mwanzo kina sura hamsini. Katika sura 1 hadi 11, historia ya awali juu ya binadamu inasimuliwa. Sura 12 hadi 50 inahusu historia ya kale ya Waisraeli. Hasa zinataja hadithi juu ya wazee au mababu wao, kama Abrahamu, Isaka, Yakobo na Yosefu.
0 Comments