ISAKA. Abrahamu alijiweka tayari kumtoa mwanae awe
dhabihu. Kwa sababu Abrahamu alikuwa mwaminifu, Mungu akathibitisha ahadi zake
kwa Abrahamu kwa kiapo. Hiari ya Isaka kufa kwa kumtii baba yake alichomwamuru
ni mfano wa Kristo. Ahadi zilirudiwa kwa Isaka (Mwa. 26: 3-5).
YAKOBO
alikuwa mwana wa Isaka. Ahadi
zilirudiwa kwake pia . Alikuwa na wana 12 - Reubeni alikuwa mwana mkubwa,
Benjamini alikuwa kitinda mimba. Lawi alikuwa ni mmoja ambaye makuhani
walizaliwa naye. Yusufu alipendwa mno.
YUSUFU. Akiwa kijana aliota ndoto mbili
zilizoonyesha picha kuwa yeye ni mtawala juu ya ndugu zake.Wakamwonea wivu,
wakamuuza kama mtumwa katika nchi ya Misri. Huko akawa mtawala, akapanga
kukusanya nafaka za kutumia wakati wa miaka saba ya njaa iliyoikumba nchi,
wakati wa kipindi hiki, Yakobo na wanawe wakaja kuishi na Yususfu katika nchi
ya Misri. Wao na watoto wao wakaishi sehemu ya Gosheni, sehemu ya Misri. Farao
aliyekuja baadae akawatesa watu wa Israeli, kwa kuwafanya watumwa.
MUSA akazaliwa wakati huu; akiwa mtoto
mchanga alifichwa katika kikapu, na kisha kukutwa na binti wa Farao na
akafanywa kuwa wake wakati akiwa kijana, akamuua Mmisri aliyekuwa anampiga
mwisraeli. Ndipo Musa akakimbilia Midani, ambako alifanya kazi ya kulisha
wanyama kwa miaka 40 kwa Yethro.Ndipo Mungu akamtokea katika kijiti kilichokuwa
kinawaka moto. Akaambiwa aende kwa Farao na kutaka ukombozi wa Israeli.
Alifanya ishara za miujiza ili kuthibitisha kuwa ametumwa na Mungu. Walakini
Farao hakuwafungua Israeli waondoke, basi mapigo kumi yalitumwa juu ya Misri,
yaani Vyura, giza, Mvua ya mawe, na mwishowe kuua kila mzaliwa wa kwanza
mwanaume. Israeli ilibidi wachinje mwana kondoo na kunyunyiza damu juu ya
milango yao. Hii ilionyesha tukio moja mbele jinsi damu ya Yesu inavyoweza
kutuokoa toka mauti. Siku kuu hii ilikuja julikana kuwa Pasaka .
KUTOKA. Hatimaye Israeli waliachwa waondoke
Misri - walisafiri huku wakiongozwa na malaika wa Mungu katika nguzo ya wingu
wakati wa mchana, na nguzo ya moto wakati wa usiku. Jeshi la Farao lilifuata
nyuma yao mpaka Bahari ya shamu. Kwa miujiza maji yaligawanyika ili watu
wapite, kisha maji yalirudi mahali pake na kuua wamisri. Ndipo wakasafiri
kupita jangwani kuelekea nchi ya ahadi ya Kanaani. Mungu aliwapa maji ya kunywa
toka kwenye mwamba, na mkate kwa namna ya mana walipewa kila asubuhi.
Walipofika mlima Sinai, Mungu akawapa amri kumi na sheria ya Musa. Wakati huo
wakawa ni ufalme wa Mungu. Wakaamriwa kufanya hema maalum, waliita hema ya
kukutania ambapo Mungu aliabudiwa. Walipewa kuhani mkuu na makuhani ambao
wanaweza kutoa dhabihu kwa Mungu. Asili yote ya hiyo masikani na ukuhani
vililenga mbele kwa ujio wa Yesu.
NCHI
YA AHADI hatimaye
waliisogelea, Wapeleezi 12 walitumwa, kumi kati yao walirudi wakisema ni vigumu
kuimiliki nchi ya Kanaani. Wapelelezi wengine wawili Yoshua na Kalebu, walisema
ukweli - kwamba nchi wataitamalaki, ikiwa wanaamini ahadi za Mungu. Kwa sababu
watu walishiriki mwenendo wa wapelelezi kumi, Israeli ikabidi wazunguke
jangwani kwa miaka 40 hata wale wote waliokuwa na umri wa miaka 20 na zaidi
walipotoka Misri walipokufa.
0 Comments