TULIKOTOKA NI MBALI
Mwimbaji: Ambwene Mwasongwe
Mwimbaji: Ambwene Mwasongwe
Tulikotoka
ni mbali, tukitazama nyuma
Asingekuwa
Bwana, tusingefika hapa
Yale
tuliyoyapitia, hayakutuacha tulivyo
Haikuwa
rahisi, ni mkono wa Bwana
Mengine
yalikuja kama mema, mwisho ukawa mbaya
Mengine
yalikuja kama mabaya, kumbe yana kusudi
Lakini
katika yote hayo, tulikuona Bwana
Ukitetea
maisha yetu, dhidi ya hatari mbaya
Tulikutana
na hatari mbaya, tukajua ni mwisho
Tulikutana
na majanga mengi, tukajua hakutakucha
Lakini
katika yote hayo wewe ulisimama
Tags
GOSPEL LYRICS