Gospel Lyrics: Watoto Yatima (Ambwene Mwasongwe)

WATOTO YATIMA
Mwimbaji: Ambwene Mwasongwe



Ilitokea hawakupenda, ndio mzunguko wa maisha
Na kama halingekuwa fungu, wasingechagua
Wanahangaika, wanateseka
Wanapata shida, hawana tumaini
Wameshaachwa, wako peke yao
Mungu watazame, kama baba yao

Wanakutegemea wewe, wanakutazama Bwana
Kilio wanacholia, wanalilia moyoni
Maana hata wakilia, nani atawafariji
Mungu uwasaidie, uwatie moyo
(Mzigo uwe mwepesi ×2)

Jamii imewasahau, wanahangaika
Hata wakiombaomba, wanawafukuza
Wengine wanawatukana, kuwaita chokoraa
(Mungu uwakumbuke ×2).

Bwanaaaaa......

CHANZO: Watoto Yatima



Post a Comment

Previous Post Next Post