UNAMKUMBUKA WILLIAM BRANHAM?

WILLIAM MARION BRANHAM
W.M Branham alizaliwa 1909. Alikuwa Mchungaji wa Waumini wa Baptist nchini Marekani. Mei 7, 1945 Branham alitokewa na Malaika. 


Akamwambia
"Usiogope natoka kwa Mungu kukupasha habari kwamba Mungu amekutuma kupeleka uponyaji kwa ulimwengu. Ukiwa mnyofu wa moyo na kuvuta watu kukusadiki, hakuna kitakachosimama mbele ya sala zako, hata ugonjwa wa kansa".

Toka siku ile Branham hakukosa kuwa na uongozi wa malaika huyo katika kazi yake. Akaanza kuhubiri na kuendesha ibada za uponyaji, maelfu ya watu wakamsikiliza na wengine wakaponywa  maradhi yao.

Maajabu mengi yakatokea wengine wakaponywa maradhi yao. Maajabu mengi yakatokea kipaji cha pekee alichokuwa nacho kilikuwa kutaja ugonjwa na hata dhambi zilizofichika za watu ambao hawahi kuwafahamu.

Katika mahubiri yake akanza kubashiri kwamba utawala wa miaka 1000 utaanza mwaka 1977 (taz. Laodecian Church Age. ukurasa 3) na kuhubiri kwa JINA LA YESU TU.

Branham akafariki siku ya Krismasi, mwaka 1965 kutokana na jeraha kichwani kama alivyotabiri. Wafuasi wake hawamkuzika mara moja bali walitayarisha mwili wake kwasababu walingoja uamuzi kutoka kwa mke wake aliyejeruhiwa na kuzimia katika ajali hiyo. Lakini pia baadhi yao walitazamia atafufuka, Januari 25, 1966, mwanzo kupiga kampeni kubwa ya kueneza INJILI, jambo hilo halikutokea siku hiyo wala ya pasaka ya mwaka 1966, na uamuzi ulifikiwa wa kumzika baada ya Pasaka huko Jeffersonville nchini Marekani.

Wafuasi wake wanamtazama Branham kama Nabii anayetangaza ujio wa pili wa Yesu kama Yohana Mbatizaji alivyotangaza ujio wa Kristo mara ya kwanza. Ndiye Nabii anayewafunulia mafumbo yaliyofichika.

KWA TAARIFA YAKO.
Nchini Tanzania ujumbe wa Branham uliingia mwaka 1971 na ndugu Isaya Mwangoka aliporudi kutoka Ulaya, kwa  kawaida  wanatunza mahubiri yake kwa njia ya mikanda au vijitabu .

MSIMAMO WA IMANI
Wafuasi wa Branham wanajikita katika Biblia tu na kukataa kila pokeo , pia hawatambui dhehebu lolote kuwa kanisa la kweli.

i.            UTATU- Mungu ni mmoja, siyo katika umoja wa nafsi 3. Ni Mungu mmoja katika hali ya utatu, Mungu juu yetu, Mungu pamoja nasi na Mungu ndani yetu.
ii.            DHAMBI YA ASILI- Ndiyo mzao wa Shetani aliyemzaa kwa kumjua Eva.
iii.            UBATIZO-Wana batiza watu wazima kwa jina la Bwana Yesu tu, kwa kumzamisha mwamini mara moja. pia hawana Askofu bali wazee ambao wanafanya kazi ya Wachungaji.

Hii ni kwa ufupi kuhusu Aliyejulikana kama William Marion Branham wa nchini Marekani.

Post a Comment

Previous Post Next Post