Tanzania Assemblies of God (TAG)
ni Kanisa lililotokana na uamsho mkubwa ulioanza huko mtaa wa AZUSA, California
(Marekani), mwanzoni mwa karne ya 20.
Deer ambaye awali alikuja
kama Mmisionary wa kujitegemea, na alianzisha Kanisa la Pentecoste Holiness
Association (PHA) mnamo mwaka 1928 ambapo ibada ya kwanza hasa ya Kanisa hilo
lilianza mapema mwaka 1929 huko Igale, Mkoa wa Mbeya.
Mnamo mwaka 1938 Paul Derr
alirejea Marekani na mwaka uliofuata 1939 alijiunga na Kanisa la Assemblies of
God, na hivyo kuikabidhi kazi iliyokuwa imeanzishwa Tanzania (wakati huo
ikiitwa Tanganyika) mikononi mwa Genenral Council ya Assemblies of God
Marekani. Na kuuomba uongozi huo wampeleke Mmissionari kwenye kazi hiyo kuilea
wakati yeye akiwa likizoni.
Historia inatuonesha kuwa
katika miaka ya mwanzo kanisa
lilisimamiwa wamishenari wa kimarekani, wachungaji wa kiafrika wakati huo, Yohana Mpayo (Marehemu) na Petros, walikuwa maaskofu chini ya Assemblies of God Mission.
Kanisa liliendelea
kuongozwa katika mfumo huo hadi mwaka 1967. Kanisa la kwanza kabisa la TAG
lilikuwapo pale Igale, Wilaya ya Mbalizi, Mkoa wa Mbeya.
Ni mwaka huo wa 1967,
uongozi wa Assemblies of God Mission, uliamua kulikabidhi kanisa kwa uongozi wa
wenyeji na Mchungaji Immanuel Lazaro, alichaguliwa kuwa Askofu Mkuu wa kwanza
mtanzania wa kuongza Tanzania Assemblies
of God (TAG).
Kanisa hili liiingia hapa
nchini kama matokeo ya uamsho mkubwa wa Kipentekoste uliotokea kule Azuza
Marekani.
Hivyo malengo makuu ya
kuanzishwa kwa kanisa ni kuwafikia wenye dhambi kwa injili iliyo hai, iletayo
wokovu na kuleta uamsho mkubwa wa Bwana wetu Yesu Kristo nchini Tanzania.
Ili kutimiza malengo hayo ilikuwa
lazima watendakazi shambani mwa Bwana waandaliwe tangu utoto wao.
Tags
WASIFU