Na Johson Jabir
MBEYA, TANZANIA
Mkanganyiko umeendelea kujitokeza kwa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma katika masuala mbalimbali likiwemo la namna anavyooa.
Imefahamika Rais Jacob Zuma (68) anatarajia tena kumuoa mwanadada Gloria Bongi Ngema mwaka 2011.
Takribani majuma mawili yaliyopita Zuma alimwoa Thobeka Mabhija (37) na sherehe hizo zilifanyika Nkandla.
Habari kutoka nchini humo zinasema Zuma na mwanadada Gloria wana mtoto mwenye umri wa miaka 3 na wakati akimwoa Thobeka Januari 4, mwaka huu, familia ya Zuma ilitoa zawadi kwa familia ya Mabhija, ambayo kwa Kizulu huhesabiwa kama mtu ameshalipiwa mahari (ilobolo).
Mwaka 2002 Zuma alitoa ng’ombe 10 kama mahari kwa mjukuu wa Mfalme Sobhuza III Sebentile Dlamini japokuwa sherehe za kumchukua hazikufanyika.
Hata hivyo wachunguzi wa mambo wanajiuliza kama kweli Rais huyu ataweza kuvipiga vita vizuri dhidi ya ugonjwa hatari wa UKIMWI katika taifa hilo.
Pia kiongozi wa chama cha Christian Democratic (CDP) nchini humo amemwelezea Rais Zuma kuwa kitengo cha kuoa wanawake wengi kinaashiria nyakati za giza, hofu ya Mungu moyoni imeondoka.
Rais Jacob Zuma ni baba wa watoto 19.