MCHUNGAJI AHUKUMIWA KUJIHUBIRIA

Mchungaji wa kanisa moja la Cincinnat, Ohio nchini Marekani amehukumiwa adhabu ya kujihubiria Neno la Mungu yeye mwenyewe baada ya kupatikana na hatia kutembeza ubabe barabarani.


Mchungaji Thomas Howell umri wa miaka 71, alikumbanana hukumu hiyo baada ya kufikishwa mbele ya Jaji wa mahakama ya Hamilton kwa kosa la kutishia kumlipua kwa risasi dereva mmoja aliyelipita gari lake.


Katika hati ya mashitaka iliyosomwa mahakamani, ilidaiwa kuwa Mchungaji Thomas, alipandwa na hasira na kuchomoa bastola yake baada ya gari moja dogo kumpita kwenye barabara yenye msongamano wa magari na kusababisha gari alilokuwa akiendesha kuyumba.


Baaada ya kuchomoa bastola, mchungaji huyo mzee alianza kuizungusha mkononi huku akililenga gari hilo kitendo ambacho kilisababisha dereva wa gari liliompita asimamishe gari lake bila kupenda na kwenda kumuomba msamaha mtumishi huyo wa Mungu.


Ikitoa hukumu hiyo juu ya mkasa huo, mahakama imemeshutumu mchungaji Thomas kwa kushindwa kuzuia hasira na imemtaka atumikie adhabu ya kujihubiria Neno la Mungu mara tatu kwa siku na kuitumikia jamii kwa kuihubiria kwa saa mbili kwa siku kwa muda wa wa saa 100.

Post a Comment

Previous Post Next Post