ASILI
YA DHAMBI
Inabidi
kusisitiza kwamba dhambi hutoka ndani yetu. Ni kosa letu hata kutenda dhambi.
Bila shaka, ingekuwa vema kuamini kuwa halikuwa kosa letu hata tukitenda
dhambi. kwa hiyari tungetenda dhambi na halafu kutoa udhuru wenyewe kwa
kuwaza kwamba kweli lilikuwa kosa la Ibilisi na ya kuwa lawama kwa dhambi
yetu ingewekwa kabisa juu yake.
Sio ajabu sana kwamba katika kesi ya mwenendo
mbaya sana, mtu mwenye kosa anaomba msamaha kwa kuwa anasema ya kwamba
alishikwa na shetani kwa muda na kwa sababu hii yeye mwenyewe hahusiki.
Lakini ni sawa kabisa, udhuru huu dhaifu unahukumiwa kwa sababu hauna msingi
kabisa, na mtu anapotishiwa hukumu juu yake.
Tukumbuke
kuwa "mshahara wa dhambi ni mauti" (Rum. 6:23);
dhambi huleta kifo. Kama sio kosa letu kutenda dhambi, bali ni Ibilisi, Bali
Mungu mwenye haki yampasa amwadhibu Ibilisi kuliko sisi. Lakini ukweli ni
kwamba tunahukumiwa kwa ajili ya dhambi zetu wenyewe yaonyesha tunahusika kwa
dhambi zetu.
Wazo la kwamba Ibilisi ni mtu dhahiri aliye nje yetu kuliko
kwamba ni jambo la dhambi ndani yetu ni kujaribu kuondoa kuhusika kwa ajili
ya dhambi zetu. Lakini huu ni mfano mwingine watu wanapokataa kupatana na
Biblia inapofundisha kuhusu mwili wa binadamu: huo kwa asili ni wenye dhambi.
"Hakuna
kitu kilicho nje ya mtu ambacho kikimwingia chaweza kumtia unajisi ….. Kwa
maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, Uasherati, wivu, uuaji,
uzinzi, tamaa mbaya ….. kiburi, upumbavu: haya yote yaliyo maovu yatoka ndani,
nayo yamtia mtu unajisi"(Marko. 7: 15 -23).
Wazo
la kwamba kipo kitu fulani nje yetu kinachotuingia na kutusababisha kufanya
dhambi halilingani na mafundisho yaliyo wazi ya Yesu hapa. Toka ndani, ya
moyo wa mtu, hutoka yote haya mambo mabaya. Hii ndiyo sababu wakati wa
gharika, Mungu aliona kwamba "mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya
tangu ujana wake"(Mwa. 8:21. Yak. 1:14)
anatuambia namna tunavyojaribiwa:"Kila mmoja (yaani mwanadamu)
hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa" Tunajaribiwa
kwa tamaa zetu wenyewe, mawazo yetu mabaya; sio kitu kingine chochote nje
yetu. "Vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyo kati yenu" ?.
Yakobo
anauliza; "Si humu katika tamaa zenu ?" (Yak. 4:1).
Kila mmoja wetu ana majaribu yake binafsi. yanazalishwa na nia zetu mbaya,
kwa sababu ni yetu wenyewe. ukweli umesemwa ya kwamba sisi wenyewe ndio adui
zaidi mbaya.
Kitabu
cha Warumi kwa upana kinahusika na dhambi, asili yake, na jinsi ya kuishinda.
Ni muhimu sana kwamba Ibilisi na shetani hawapatikani sehemu walipotajwa
katika kitabu hiki; kwa maneno ya kusema kuhusu asili ya dhambi, Paulo
hamtaji Ibilisi au shetani. Kwa njia hiyo hiyo'Ibilisi’ ni dhana ya Agano
Jipya.
Kama yupo kiumbe aliye nje anayefanya tutende dhambi, kwa kweli
asingetajwa kwa upana katika Agano la Kale ?. Bali upo ukimya wa maana
uliokwenda chini kuhusu hili. Taarifa ya kipindi cha waamuzi au Israeli
jangwani, zinaonyesha ya kwamba nyakati hizo Israeli walitenda dhambi sana.
Lakini Mungu hakuwaonya kuhusu kiumbe mwenye nguvu kuwa atawaingia na
kuwafanya watende dhambi. Badala yake, aliwasisitiza kushika neno lake, ili
wasivutwe kwenda nje ya mapenzi yake na kuufuata mwili wao (K/Torati
27:9,10; Yoshua 22:5)
Paulo
analia:"Ndani ya mwili wangu halikai neno jema …. Kutenda lililo jema
sipati ….. Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi
yangu nilitendaye, bali ile dhambi ikaayo ndani yangu"(Rum. 7:18 -21).
Kutenda kwake dhambi hamlaumu kiumbe aliye nje aitwaye Ibilisi. Anaweka
kwenye mwili wake mbaya kuwa ndiko asili ya dhambi:"Sio mimi nafsi
yangu, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu".
Basi, nimeona sheria hii
(ndani yangu), ya kuwa kwangu mimi nitakaye kutenda lililojema, lipo lililo
baya (yaani - ndani) yangu. Hivyo anasema kwamba kipingamizi cha kuwa kiroho
kinatoka kwingine anapoita"dhambi ikaayo ndani yangu". kila mtu
mwenye mawazo ya kunia kiroho atafikia kwenye mawazo hayo hayo. Ijulikane ya
kwamba hata mkristo mkubwa kama Paulo hakuona badiliko la mwili baada ya
kuongoka, wala hakuwekwa kwenye nafasi ambayo hawezi kufanya dhambi.
Makundi
ya siku hizi ya "Kiinjili" yanadai kwamba wapo katika nafasi hii ya
kutotenda dhambi, kwa hivyo wanamweka Paulo vema ndani ya 'wasiookoka’ kwa
sababu ya taarifa yake hapa katika Rum. 7: 15 -21. Mistari hii
imewaletea shida kubwa kwa madai yao. Daudi, mwingine pasiposhaka mtu mwenye
haki, vivyo hivyo alifafanua juu ya mwili wake kabisa mwelekeo wa daima wa
dhambi: "Tazama mimi naliumbwa katika hali ya uovu, mama yangu
alichukuwa mimba hatiani - dhambini"(Zab. 51:5).
Biblia
ipo wazi kabisa kuhusu ukubwa na ubaya wa mwili wa binadamu. Kama hili
likikubalika, hakuna haja ya kutafuta mtu wa kufikiriwa aliye nje ya
mwanadamu anayehusika na dhambi zetu. Yer. 17: 9 unasema kwamba
moyo wa binadamu huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote ambapo hauwezi hasa
kukubali upana mbaya sana wa dhambi zake.
Naye Yesu alitia alama pia mwili wa
mwanadamu kwa asili ni mbaya katika Math. 7:11; Mhubiri 9:3
(andiko la Kiebrania) halikuweza kuwa wazi;"Moyo wa wanadamu umejaa
uovu", Efe. 4:18 inatoa sababu ya mtu asili ya kutengwa
toka kwa Mungu kuwa ni "kwa sababu ya ujinga uliomo ndani yao, kwa
sababu ya ugumu wa mioyo yao". Ni kwa sababu ya upofu wa kiroho na
ujinga wa mioyo, njia zetu za kufikiri zilizo ndani yetu, ndizo zimetuweka
mbali na Mungu.
Pamoja na mstari huu, Gal. 5:19 unasema dhambi
zetu kuwa ni"Matendo ya mwili"; ni mwili wetu wenyewe, utu wetu
kabisa na umbo, ndivyo hutufanya tutende dhambi. Hakuna hata fungu la maneno
linaloeleza asili ya dhambi ndani yetu kuwa zimekuwemo kwa sababu ya Ibilisi
aliyeziweka; maelekeo ya dhambi ni mambo mengine ambayo kwa kawaida tunayo
tangu kuzaliwa; ni sehemu kubwa ya umbo la mwanadamu.
|
Tags
MASWALI NA MAJIBU