Krismasi Njema


Desemba 24 kila mwaka katika utamaduni wa Magharibi huwa maalum kwa kile kinachofahamika kama watoto kupokea zawadi kutoka kwa ‘Santa Claus’ au ‘Father Christmas’. Tukio hilo hufanyika siku moja klabu ya Desemba 25. 
Santa Claus (pichani) hujulikana kwa kuwa na ndevu nyingi katika kidevu, koti jekundu lenye upindo mweupe shingoni, suruali nyekundu na viatu vya vyeusi bila kusahau mkanda mweusi kiunoni.

Aidha ‘Father Christmas’ hubeba mfuko mkubwa uliojaa zawadi kwa ajili ya watoto.

‘Santa Claus’ inaaminika alikuwa na orodha ya watoto wote duniani na tabia zao kama ni mtoto mwenye adabu au mtovu wa nidhamu, hivyo wakati wa ugawaji wa zawadi alikuwa akitoa kulingana na tabia za watoto.

Kabla ya mwaka 1823 katika nchi za Marekani na Canada, Santa Claus alikuwa hana kidevu kilichojaa ndevu lakini shairi lililotungwa wakati huo la ‘A Visit From St. Nicholas’ na mchoraji wa vikaragosi Thomas Nast alimchora  ‘Santa Claus’ akiwa na ndevu na ‘moustache’.

Jina ‘Father Christmas’ lilianza kutumika katika karne ya 16 nchini England wakati wa utawala wa Mfalme Henry VIII wakati alipochorwa na kuonekana kama mtu mkubwa akiwa kwenye mavazi ya kijani.

Mchoro huo ulimuonesha Henry VIII kama mtu mwenye roho nzuri, mpenda amani, mleta furaha katika jamii, anayependa chakula kizuri na mvinyo.

Hivyo wakaanza kusheherekea Sikukuu ya ‘Saint Nicholas’ Desemba 6.

Baadaye waliihamishia hadi Desemba 25 baada ya Uamsho wa Victoria ulioleta siku ya Christmas (kusheherekea siku ya kuzaliwa Yesu Kristo).

Feliz navidad y nuevo año felicidad’ yaani Merry Christmas na Heri ya Mwaka Mpya.


CHANZO: Jaizmelaleo

Post a Comment

Previous Post Next Post