Maana ya ‘motivational speaker’
ni ‘msemaji ambaye anawatia moyo watu na kuwahamasisha wafikie malengo au
makusudi yao kupitia kubadilisha mtazamo wao.
Yesu na wanafunzi wake |
Usemi au fikra ‘motivational
speaker’ inatoka wapi? Inatokana na nia na roho ya kizazi hiki ambao hawamjui
Mungu.
Nyendo au mafundisho haya
yalianza miongoni kwa wasioamini hasa kama miaka 40 iliyopita.
Msingi wa mafundisho haya ni
ifuatayo: huhitaji mtu mwingine; huhitaji Mungu au dini; wewe mwenyewe kama
binadamu tayari unao uwezo ndani yako kubadilisha maisha yako na kutimiza ndoto
zako zote na kutekeleza malengo yako yote!
Wasemaji hao wanaahidi watu
watafanikiwa katika kila eneo la maisha yao – inategemea na mtazamo na fikra
zao tu!
Ni lazima kubadilisha mtazamo
wako tu! Kama ukibadilisha mtazamo wako na fikra zako, yote yatawezekana kwako!
Kwa maneno hayo wasemaji hao (motivational speakers) wanachochea hisia za watu
ili waamini waweze kutekeleza malengo yao!
Wanahubiri maisha ya
kujitegemea kabisa! Kwa msingi, wanahubiri wewe ni mungu! Mamilioni wa
wasioamini wamefuata ‘injili’ hiyo.
Wasemaji hao wanaandika ‘Self-help’ vitabu, yaani, ‘Jisaidie
Mwenyewe’ vitabu, kama ‘10 Steps to
Success’, ‘Achieve Your Goals’, ‘Change your Destiny by Changing your
Attitude.’ (‘Hatua Kumi Kufanikiwa’, ‘Tekeleza Malengo Yako’, ‘Badilisha Maisha
Yako Kupitia Kubadilisha Mtazamo Wako’ nk.)
Bila aibu yo yote, wahubiri wa
kikristo siku hizi wanatumia maneno haya haya na lugha hiyo hiyo! Wahubiri hao
wanaigia wasemaji wale wasioamini (motivational speakers) kabisa na kupitia
mafundisho hayo wanataka kuwavuta vijana wengi sana, na wanafanya hivyo!
Hasa vijana wa kikristo huvutwa
na mafundisho hayo na wanakunywa udanganyifu huo kwa sababu yanaahidi mafanikio
na matekelezo ya malengo yao!
Kwenye Facebook unaweza kuona
wengi hufurahia udanganyifu huo. Kwenye somo hili nataka kuweka wazi kwamba
katika Biblia hakuna ‘motivational speakers’ – hata mmoja! Biblia inasema,
“…mtu mmoja alimwambia,
‘Nitakufuata ko kote utakakokwenda.’ Bwana Yesu hakujibu, ‘Oh! Nafurahi
unapenda kunifuata. Hongera! Kumbe, unavyo vipaji vizuri nami nitakutumia na
utafanikiwa!’ Bwana Yesu akamjibu kwa namna hiyo, “Mbweha wana pango, na ndege
wa angani wana viota, lakini Mwana wa Adamu hana pa kujilaza kichwa chake.” (Luka 9:57,58).
Je, unafikiri jibu hili la Yesu
lilimpendeza yule aliyejitolea? Je, maneno haya yalimtia moyo? Kwa maneno haya
Bwana Yesu alitaka kumuamsha mtu huyo aelewe kwa dhati maana ya ‘kumfuata
Yesu’!
Mtu anaweza kuwa na hamu
kumfuata Yesu bila kuelewa maana yake, bila ‘kuhesabu gharama’! Labda mtu huyo
aliamini Injili ni Injili ya ‘baraka’, yaani, labda akasema moyoni kwake, ‘Ahh,
Mungu atanisaidia sasa, atanibariki, ataniokoa kutoka katika mazingira yangu
mabaya na atayafanya maisha yangu yawe nzuri na atanisaidia kufanikiwa!’
Jibu la Yesu liliuzima moto wa
hamu ya namna hiyo; liliizima hamu yenye tabia ya kibinadamu kujifaidia!
Hapana! Injili sio jambo la kujiendeleza mimi mwenyewe, kujifurahisha
matelekezo ya malengo yangu, kuboresha ‘uwezo’ wangu, kujitajirisha!
Labda yule aliyetaka kujitolea
kumfuata Yesu alifikiri, “Kumbe, ninavyo vipaji, ninao uwezo mzuri ambazo Mungu
angeweza kuzitumia kujenga mfalme wake duniani!” Au hudhani hivyo?
Lakini nilisoma kwenye Facebook
mtu fulani (mkristo?) aliyeweka post ifuatayo kwenye group ya kikristo fulani,
“Mungu anautumaini uwezo wako, basi wewe pia unaweza kufanya vile vile.” Na
watu wengi (wakristo?) waligonga ‘like’!
Tunaongea, tunaandika kama
Biblia haipo! Watu hawajali neno la Mungu kabisa! Paulo alitanganza, “Sisi
wenyewe tulikuwa na hukumu ya mauti katika nafsi zetu ili TUSIJITUMAINIE NAFSI
ZETU, bali TUMTUMAINI MUNGU.” (2
Wakor.1:9), na tena, “Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Mungu kwa Roho, na
kuona fahari juu ya Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili (yaani, uwezo wangu
mwenyewe).” (Wafil. 3:3).
Wengi wanatangaza, ‘Usikate
tamaa! Usikate tamaa! Utafanikiwa. Songa mbele tu! Mungu atakusaida
kufanikiwa!’ Kwa nini wanasema mara nyingi ‘kufanikiwa’? Ina maana ya namna
gani?
Kufanikiwa katika biashara
yangu? Kwa nini hawatumii lugha ya Biblia? Kwa nini watu hawa hawaandiki ‘Amini
Mungu naye atakusaidia kushinda dhambi’ au ‘Usikate tamaa!
Songa mbele na utaona Mungu ni
Mwaminifu!’ Kwa nini wengi wanapenda na wanapendelea kutumia lugha ya
‘mafanikio’. Katika muktadha huo, Bwana Yesu hakutumia lugha hiyo wala mitume wake.
Bwana Yesu hatafuti watu
wajitoleao. Anatafuta watu ambao watatubu kwa ndani sana, kujikana wenyewe na
kuchukua msalaba wao. Mungu anatazamia sisi tuyatafute mapenzi Yake tu, na siyo
kuyajenga mapenzi yetu mweyewe kadiri tunavyopenda.
“Mtu mwingine pia akamwambia,
Bwana, ‘Nitakufuata; lakini, nipe ruhusa kwanza nikawaage watu wa nyumbani
mwangu.’ (Luka 9:61). ‘Nitakufuata
…lakini kwanza…’. Hamna ‘lakini kwanza’, hamna ‘lakini’. Yesu ni Mwana wa
Mungu! Huwezi kubadili na Mungu. Yesu hakufa kustarehesha maisha yetu! “Yesu
akamwambia, ‘Mtu aliyetia mkono wake kulima, kisha akaangalia nyuma, hafai kwa
ufalme wa Mungu.’” (Luka 9:62).
CHANZO:
somabiblia
0 Comments