Mbingu na dunia zilitoka wapi? Jua, mwezi na
nyota na vitu vingi duniani vilitokea namna gani? Biblia inatoa jibu la kweli inaposema
viliumbwa na Mungu.
Basi hapo tunajifunza kwamba watu wa roho ndio walioumbwa
kwanza na Mungu, wakawa kidogo kama yeye . Hao ni malaika. Lakini dunia
iliumbwa kwa ajili ya watu kama sisi.
Halafu Mungu akaumba mwanaume na mwanamke
walioitwa Adamu na Hawa (Eva), kisha
akawaweka katika bustani nzuri. Lakini hawakumtii Mungu, wakaipoteza haki ya
kuendelea kuishi.
Jumla ya miaka kutoka kuumbwa Adamu mpaka Gaharika Kuu ni
1656.
Wakati huo waliishi watu wengi wabaya. Huko mbinguni, walikuwako watu wa roho wasioonekana, Shetani na malaika zake wabaya. Hapa duniani walikuwako Kaini
na watu wengine wabaya na watu wakubwa mno.
Tags
THEOLOJIA