Kitabu cha “Historia ya Ukristo” kilichoandikwa na Deam A.
Peterson na kuchapishwa na Central Tanganyika Press, mwaka 1969 kinaeleza mengi
kuhusu historia ya ukristo lakini kubwa zaidi katika kitabu hicho anaeleza kuwa
sio watoaji wote na kila chuo cha theolojia hukubaliana na mafundisho yote
yaliyomo. Peterson ameangazia maeneo mbalimbali kama ifuatavyo;
- Hali ya Ulimwengu mwanzoni mwa Kanisa
- Kuenea na kuteswa kwake Kanisa
- Maendeleo na mabishano ya Theolojia
- Umoja na Utawala wa Kanisa
- Majadiliano ya Theolojia zamani za Mfalme Konstantino.
- Umonaki wa Kikristo
- Kanisa wakati wa ushindi wa mataifa makorofi ya Ulaya.
- Upapa wa Rumi na uenezi wa Injili
- Kanisa la Mashariki zamani za A.D 500-1000.
- Kanisa la Magharibi
Nami sitatofautiana sana na Peterson, nitaendelea kupita humo
humo katika kuendelea kutunza historia hiyo na kuongeza baadhi ya mambo
kutokana na wakati tulio nao kutoka vyanzo mbalimbali.
Maneno ya Dean A. Peterson
“Historia ya Kanisa la Kikristo yaweza kuandikwa kwa kufuata
mipango mbalimbali. Yawezekana iandikwe kueleza jinsi kanisa lilivyoenea kutoka
Yerusalemu hata pande zote za dunia. Yawezakana historia ya kanisa iandikwe kwa
kufuata mikazo na mabishano ya theolojia, kwani hayo yamo sana katika maisha
yake. Tena inawezekana tuchunguze maisha ya watu mashuhuri waliotenda makuu
katika historia ya kanisa. Njia hizo, pamoja na njia nyinginezo , huwa na faida
yao. Mwandishi wa kitabu hiki (Historia ya Ukristo), amevutwa kushirikisha njia
hizo tatu akijaribu kuonyesha historia ya kanisa kwa kufuata makuu ya uenezi
wake nay a theolojia yake kwa njia ya kuyachungulia maisha ya watu wake.
Historia ya kanisa ni habari za maisha ya watu, wakuu kwa wadogo. Katika kuona
jinsi walivyopatwa na nguvu ya Mungu katika Kristo tutapokea baraka kwa maisha yetu
ya leo. Tenakwa kuchunguza jinsi walivyoshindania maisha ya kikristo katika
mazingira katika mazingira yao tutapewa uongozi na hekima zihitajiwazo katika
ulimwengu wa leo. Ujuzi wote haumo katika kizazi chetu. Kukataa mafundisho ya
karne zilizopita ndiko kujiweka katika umaskini wa ujinga. Haya basi, tuanze
kutazama habari za mababa zetu katika Imani. Najua kwamba kitabu hiki kingefaa
zaidi kama kingeandikwa na Mwafrika. Maana usemi wake na mikazo yake ingelenga
shabaha sawasawa. Lakini kwa kuwa huyo hajapatikana kwa kazi hii mpaka sasa,
najaribu niwezavyo nikitumaini ya kuwa kitabu hiki kitaleta msaada mpaka
kingine kifaacho zaidi kitatolewa.”
Shabaha kubwa ya kukuletea masuala haya ni pamoja na kujaribu
kutunza kumbukumbu kwa njia ambazo zinaweza kuwa msaada kwa vizazi vijavyo.
Kama ambavyo wao walipambana kutunza kwa njia ya kuandika kwenye vitabu kwa
karne ya 21 tunapambana kutunza katika mtandao wa Intaneti ili watakaokuja
baada yetu au wanaotaka kujua kuhusu ukristo waweze kupata rejea mbalimbali
ambazo zitaweza kuwasaidia kupata mambo yaliyopita.
Historia ya Kanisa ambayo nitaanza kuiweka hapa itakuwa
katika maeneo makuu matatu ambao ni Historia ya Kanisa la karne ya kwanza hadi
kumi, Historia ya Matengenezo (Reformation) karne ya 11 hadi 17 na Historia ya
Kanisa katika karne ya 18 hadi 20.
HALI YA ULIMWENGU MWANZONI MWA KANISA
Tags
THEOLOJIA