VIJANA wa Kikristo katika Kanisa la Tanzania Assemblies of God Ilomba Mbeya wametakiwa kuwa kati hali ya usafi wa kimwili.
Akifundisha katika darasa la Mabalozi wa Kristo Mwalimu Joshua Matagane alisema vijana wengi wamekuwa wakijitakasa rohoni na kusahau kuwa hata mwili nao una mahitaji yake. Akitolea mfano wa vijana wa kiume alisema kuwa mara nyingi huwa hawafui nguo za ndani muda mwingine hata soksi hutoa harufu mbaya ambayo huleta kero kwa watu wengine. Hata hivyo hakuishia hapo kwa upande wa vijana wa kike alisema wakati mwingine huchelewa kuolewa kwasababu ya kutokuwa wasafi katika miili yao. Mwalimu Matagane alihitimisha kwa kuwataka vijana wote kuwa mfano kwa wengine ambao hawajampokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wao.