WATOTO WATAKIWA KUWA NA MOYO WA SHUKRANI

WATOTO chipukizi wa kanisa la Tanzania Assemblies of God Ilomba Mbeya wametakiwa kuwa na moyo wa shukrani siku zote kwani ndio Mungu awatakavyo watu wake wafanye hivyo.


Akifundisha katika darasa hilo Mwalimu Costan Mwenga alisema kuwa wengi husahau kuwa shukrani huongeza kitu katika maisha ya mtu aliyeokoka. Akitolea mfano wa wakoma walioponywa na Yesu alisema kuwa hata Yesu mwenyewe alishangaa kumuona yule mmoja akija kushukuru na kuwauliza wengine wako wapi. Hata hivyo Mwalimu Mwenga aliwataka watoto hao hata wanapokuwa majumbani mwao kujitahidi kuwashukuru wazazi kwa mambo ambayo wanawatendea na sio mpaka wakumbushwe.



Post a Comment

Previous Post Next Post