JAMVI LA HABARI ZA T.A.G ILOMBA MBEYA TANZANIA

JAMVI LA HABARI lenye kukujuza habari mbalimbali kutoka Kanisa la Tanzania Assemblies of God Ilomba Christian Centre  Mbeya linakunjuliwa tena leo Januari 15, 2011 na Johnson Jabir lakini kwanza ni Muhtasari wa habari.
·       WATOTO wametakiwa kujifunza Neno la Mungu kwa bidii kwani ndilo uzima wao.
·       Waongofu  wapya wametakiwa kulijua neno la Mungu kwani ndiko kwenye ahadi tele za Mungu.
·       WAAMINI wa kanisa la Tanzania Assemblies of God Ilomba Mbeya wametakiwa kujua kuwa Yesu Kristo ni mtawala wa haki tofauti kabisa na watawala wa dunia hii.
·       VIJANA wametakiwa kujua kuwa mafanikio sio kitu rahisi kama wengi wanavyodhani .
HABARI KAMILI…………………………………………………………………………
JAMVI LA HABARI
ZA
KANISA LA TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD  ILOMBA MBEYA JANUARI 15, 2011
WATOTO wa kanisa la T.A.G Ilomba Mbeya wametakiwa kujifunza Neno la Mungu kwa bidii kwani ndilo uzima wao.
Akifundisha katika darasa la watoto Mwalimu Filbert Chalale wa kanisani hapo alisema kuwa wazazi wengi hawaoni umuhimu wa kuwafundisha watoto wao maneno ya Mungu kutokana na kutingwa na shughuli mbalimbali.
Hata hivyo aliwataka watoto wenyewe wakifika majumbani mwao wajitahidi kusoma Neno la Mungu  kwani Neno hilo ni uzima wa maisha yao.
Pia aliwafundisha katika  Biblia kuna vitabu vya Injili  ambavyo ni Mathayo, Marko, Luka na Yohana
Katika ibada hiyo watoto 104 walihudhuria.
JAMVI LA HABARI
ZA
KANISA LA TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD  ILOMBA MBEYA JANUARI 15, 2011

Wakati huohuo waongofu wapya wa kanisa hapo wametakiwa kulijua neno la Mungu kwani ndiko kwenye ahadi tele za Mungu .
Akifundisha katika darasa hilo ambalo lilihudhuriwa na waongofu wapya 22 Mzee Felix Kyando wa kanisa hapo alisema kuwa tabia ya kusoma Neno la Mungu itawaokoa hata wakati wa shida na kuongeza kuwa Daniel alimdai Mungu ahadi baada ya kusoma Neno la Mungu.
Pia alisema kuwa kulijua Neno la Mungu kumegawanyika katika maeneo makuu mawili ambayo ni kwa kufundishwa na kujibidisha kibinafsi kama mwamini.
Hata hivyo aliwataka kutokaa kimya kwani kumezuka tabia kwa waamini wa sasa kukaa kimya hata kama wana jambo wanalotaka kuuliza lililomo ndani ya Biblia hali ambayo huwafanya kukaa kanisani kwa muda mrefu pasipo kuijua Biblia inasema nini.
Aidha alisisita kuwa kujifunza kuhitajika juhudi za makusudi ili kufanikiwa kama kuwahi kufika katika mafundisho mbalimbali na kuhudhuria vipindi vya mafundisho.
 JAMVI LA HABARI
ZA
KANISA LA TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD  ILOMBA MBEYA JANUARI 15, 2011

WAAMINI wa kanisa la Tanzania Assemblies of God Ilomba Mbeya wametakiwa kujua kuwa Yesu Kristo ni mtawala wa haki tofauti kabisa na watawala wa dunia hii.
Akifundisha somo katika Shule ya Uanafunzi Jumapili iliyopita kanisa hapo Mwalimu Furahia James alisema kuwa wengi hushindwa kumtofautisha na watawala  wa dunia hii kama marais, wabunge na wengine kwa kumuona kuwa  yupo sawa nao kitu ambacho sio sahihi
Aliongeza kusema kuwa Yesu hafananishwi na yeyote yule kwani hata alipokuwa katika hali ya ubinadamu hakutenda dhambi pekee sasa itakuwaje alinganishwe na watawala ambao wapo katika ulimwengu huu.
Hata hivyo aliwataka waamini wa kanisani hapo kutambua kuwa kumwamini Yesu ni kuzuri kwani kutawaongoza kumfikia Mungu katika haki na kusisitiza kuwa hizi ni nyakati za mwisho za ujio wake Kristo Yesu hivyo kila mtu hapa duniani akae mkao wa kumpokea  kwa Yule ambaye hajamwani Kristo amwamini.
Katika ibada hiyo walihudhuria waamini 245.
 JAMVI LA HABARI
ZA
KANISA LA TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD  ILOMBA MBEYA JANUARI 15, 2011

VIJANA wa kanisa la Tanzania la Assemblies of God Ilomba Mbeya wametakiwa kujua kuwa mafanikio sio kitu rahisi kama wengi wanavyodhani .
Akifundisha  katika darasa la Mabalozi wa Kristo kanisani hapo Mwalimu Aminika Mwihomeke alisema kuwa mafanikio huja kwa kuongeza bidii katika kazi yawe mafaniko ya kiroho  na kimwili.
Aliongeza kwa kusema kuwa Mungu anaweza kukuonyesha mafanikio lakini asikuonyeshe njia ya kufikia hivyo mwamini akiongeza bidii basi mafanikio atayaona .
Hata hivyo aliweza kuhoji kwanini mitihani ya taifa hapa nchini Tanzania inavuja na kusema kuwa kuvuja kwa mitihani hiyo kunatokana na vijana kujibweteka kutaka mafanikio bila ya kutoa jasho .
Aidha Mwalimu Mwihomeke alisema kuwa katika kuyapata mafanikio sio lazima watu wakuunge mkono katika lile ulifanyalo kwani imebainika kuwa wengi hupenda kuungwa mkono kwa kila jambo wanalolifanya hapo ndipo mfano wa Yusufu alipoutolea kuwa Mungu alimuonyesha mafanikio yake lakini ndugu zake hawakufurahia kabisa.
Katika Ibada hiyo walihudhuria vijana takribani 55.  

 JAMVI LA HABARI
ZA
KANISA LA TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD  ILOMBA MBEYA JANUARI 15, 2011

MCHUNGAJI na Mwalimu wa kanisa la Tanzania Assemblies of God Ilomba Mbeya Vinac Amnon Mwakitalu amewataka wakamini kanisani hapo kutambua kuwa  maombi ni suala amablo halitakiwi kupuuzwa hata kidogo.
Akihubiri katika ibada ya kwanza na ya pili Jumapili iliyopita alisema kuwa kama ilivyo kwa Neno la Mungu kukaa katika  moyo wa mwamin ndivyo inavyotakiwi kwa maombi kuwa kitu cha kudumu katika maisha ya mkristo.
Aliongeza kusema kuwa maombi ni sauti inayokwenda moja kwa moja kwenye sikio la Mungu na kudai kuwa kama kanisa litaacha kuomba basi ni kumwambia Mungu kuwa aache kufanya katika maisha ya mwanadamu.
Pia alisema kuwa maombi hubadilisha watu na ulimwengu kwa ujumla wake huleta mapinduzi .
Hata hivyo aliwataka wakristo hao kutofautisha kati ya kuamuru na kuomba kutokana na dhana potofu kusambaa katika fikra za waamini hapa nchini kuwa anapoamuru vitu vitu anasema kuwa anaomba kumbe sio hivyo.
Aidha alitoa wito kwa waamini hao kuacha mara maombi ya kijeshi kwani Yesu mwenyewe hakuwa na maombi ya kijeshi, alipotaka kuomba alitafuta utulivu na kuanza kupeleka haja zake kwa Mungu Baba na sio kuamuru kama wengi wanavyodhani.

JAMVI LA HABARI lenye kukujuza habari mbalimbali kutoka Kanisa la Tanzania Assemblies of God Ilomba Christian Centre  Mbeya LA JANUARI 15 MWAKA HUU LINAKUNJWA SASA KWA MUHTASARI WA HABARI NA LITAKUNJULIWA TENA JUMA LIJALO PANAPO MAJALIWA.




Post a Comment

Previous Post Next Post