UANDISHI WA VITABU NA CHANGAMOTO ZAKE KWA KANISA LA TANZANIA.

Neno “uandishi” ninapoanza kulitamka tayari kwa kizazi hiki cha utandawazi kinakimbilia kwenye kadhia ya vyombo vya habari.
MCHUNGAJI ERNEST NGUVILA
MCHUNGAJI NGUVILA AKIONGEA NA ASKOFU MBETWA 
Lakini leo ninaataka kuzungumzia hasa katika “uandishi wa vitabu”, ninahama kutoka “uandishi katika vyombo vya habari” kama redio, magazeti, majarida, televisheni na wavuti na kutuama katika VITABU na changamoto zake kwa kanisa.


Kuna waandishi wengi hapa ulimwengu tangu kadhia hii ilipoanza lakini kihistoria inaonyesha kukua kutoka hatua moja hadi nyingine kulingana na teknolojia ya kizazi kilichopo kwa wakati huo na kutofautianaa na teknolojia ya kizazi kilichopita na kitakachokuja.


Mwandishi wa blogu ya MCRCTV (http://www.mcrctv.blogspot.com/) Jabir Johnson alifanya mahojiano na Mtafsiri wa Vitabu kutokaa lugha ya Kiingereza kwenda Kiswahili; na Kiswahili kwenda lugha ya Kiingereza Mchungaaji na Mwalimu Ernest Nguvilawa Huduma ya BSEF ya Jijini Mbeya kuhusu uandishi wa Vitabu na changamoto zake kwa kanisa hasa ukizingatia watumishi wengi wa Mungu nyakati za leo nchini Tanzania wamejikita kuandika vitabu mbalimbali; vyenye ujumbe wa Neno la Mungu kwa kanisa.


MCH. NGUVILA
Ni kweli karne ya 21 imeanza kwa nguvu kubwa sana katika kadhia hii ya uandishi wa vitabu, majarida n.k kwa upande wa kanisa; hii inaonyeshaa wakristo wenyewe na watumishi wa Mungu kufunguka katika suala zima la kujisomea licha ya kwambaa ni kwa kasi ndogo.


MCRCTV
Licha ya nguvu kubwa ya uandishi wa vitabu nini sababu hasa zinazofanya kuwa katika kasi ndogo ya usomaji wa vitabu hivyo


MCH. NGUVILA
Kwanza naweza kusema; uelewa mogo wa waandishi wa vitabu na pia wasomaji. Pili utandawazi-umesababisha wakati mwingine vitabu hivyo visisomwe kutokana na teknolojia ya mawasiliano kuwa chini kwa pande zote mbili, nikiwa na maana kwa wachungaji na wasomaji kwani wenye uelewa na teknolojia ya mawasiliano ni wachache.


MCRCTV
Hili suala la uelewa mdogo wa waandishi wa vitabu na pia wasomaji huoni kwa kulizungumza hadharani unaendelea kushusha ari miongoni mwao.


MCH. NGUVILA
Hapana; sishushi morali kwa pande zote bali ni ukweli usiopingika kwamba kuna wakati baadhi ya waandishi wamekuwa wakiandika kazi zao katika kiwango cha chini kutokana na kutofuata sheria za uandishi wa vitabu kuanzia hatua za mwanzo hadi kinapotoka.


Waandishi wengi wa vitabu nchini Tanzania wanapoandika vitabu vyao hukosa ISBN-International Serial Book Number; kwa kujua ama kutojua wamejikuta wakitoa kazi katika kiwango chaa chini na msomaji kwasababu ya uelewa mdogo anapokea kama kilivyo na makosa hatimaye migongano inaanza ndani ya jamii.


Ukweli ni kwamba waandishi wengi hukurupuka katika kuandikaa vitabi hivyo bila kujipanga hatimaye soko lake kuwa chini.


MCRCTV
Tukirejea sasa katika kutafsiri maandiko katika vitabu kutoka lugha moja kwenda nyingine hasa katika lugha hizi mbili Kiswahili na Kiingereza unakutana na changamoto gani katika kadhia hiyo kwa waandishi wa vitabu vya kanisa; yaani vyenye ujumbe wa Neno la Mungu.


MCH. NGUVILA
Changamoto ni nyingi kwa uchache ni kwamba muda wa kutafsiri hutakiwa kuwa mrefu kwa haraka na kwa umakini mkubwa ili kuepusha kupotosha maana iliyokusudiaa.


Pia waandishi wa vitabu hivyo wakati mwingine hujikuta wakiweka na mambo ya Mila na Desturi za kwao hivyo mtafsiri anatakiwa kuwa na ufahamu zaidi kuhusu tamaduni na wakati mwingine hulazimika kubadilisha baadhi ya mifano ili iwafae watu wa jamii inayopelekewa.
Wakati mwingine watumishi wa Mungu ambao ndio waandishi wa vitabu ni wagumu kushauriwa kwenye baadhi ya masuala kuhusu vitabu vyao kwa kujua ama kutojua huona kama mtafsiri anataka kupotosha amaana aliyokuwa akiitaka.


Johnson Jabir


Januari 2012


Post a Comment

0 Comments