Pastor Ikera, ‘Heavy Weight’ uthibitisho wa Nguvu za Mungu kwa njia ya Miujiza Kilimanjaro


MTOTO hulia kwa uchungu sana kitu cha kuchezea anachopenda kinapoharibika. Kilio chake huhuzunisha sana! Lakini je, umewahi kuona jinsi mtoto anavyosisimuka mzazi anapokirekebisha kitu hicho na kukirudisha katika hali nzuri?

Yehova ambaye ni Baba bora zaidi, ana uwezo wa kurudisha katika hali nzuri vitu na hali mbalimbali ambazo watoto wake wa kidunia huenda wakadhani haziwezi kuboreshwa.

Nabii Isaya alitabiri kuhusu wakati ambapo wagonjwa, walemavu, vipofu, na viziwi wataponywa na hata kifo kitamezwa milele. (Isaya 25:8; 35:1-7) Ahadi hizo hazikutimizwa kihalisi katika Israeli la kale. 

Na ijapokuwa tumeona ahadi hizo zikitimizwa kwa njia ya kiroho nyakati zetu, kuna msingi thabiti wa kuamini kwamba ahadi hizo zitatimizwa kihalisi na kikamili wakati ujao.
Pastor Peter Ikera
Mkoani Kilimanjaro Pastor Peter Ikera wa Kanisa la Enlightened Christian Gathering Church of Tanzania (ECG) lililopo Rau jirani na 5gb Resort  mjini Moshi  amekuwa akitumiwa na Mungu kufikisha ujumbe wake kwa watu na kuteka hisia za wengi na matokeo yake ni kuonekana kwa mamia ya walioachia mioyo yao itembelewe na Bwana Yesu.

UPONYAJI WA MWANAMKE ALIYEPOOZA
Mwanamke aliyekuwa ameugua na kupooza kwa zaidi ya miaka minne amepokea uponyaji kutoka kwa Mungu kupitia mtumishi wake Pastor Peter Ikera.

Akiwa hawezi kunyanyuka kitandani, ndugu jamaa na marafiki ndio waliokuwa wakihangaika naye kumpa huduma mbalimbali hadi pale alipoombewa na kuweza kupokea uponyaji uliomtoa katika vifungo hivyo.

Akitoa ushuhuda katika Ibada, Mama huyo anayefahamika kwa majina ya Hilda Mlay, Mkazi wa Mwika alisema “Nina miaka Minne nikisumbuliwa na ugonjwa huu.”

Mama huyo alisema kitu  ambacho kimekuwa cha tofauti kwa mtumishi huyu wa Mungu, Pastor Ikera ni ule wakati ambapo huanza kutabiri kwa Roho wa Mungu na kuanza kusema mambo yaliyofichika na kufungua maisha ya watu wengi kwa kipawa cha unabii.

Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la (ECG) tawi la Kilimanjaro, Pastor  Peter Ikera akifahamika kwa jina maarufu, 'Heavy Weight', amefanikiwa kuukamata mkoa wa Kiliamanajro, kwa Injili inayoambatana na miujiza na matendo makuu ya Mungu.

USHUHUDA WA UPENDO LYATUU, MKAZI WA BOMA NG’OMBE
Akizungumza Dada mmoja aliye fahamika kwa majina Upendo Lyatuu wa Boma ng'ombe Kilimanjaro, Jumapili iliyopita kuwa mtumishi wa Mungu ambaye ni mwana wa kiroho wa nabii Shepherd Bushiri pastor Ikera alimtabiria mwaka jana tarehe 1/4/2018, kuwa alimwona akihangaika kujenga nyumba bila mafanikio na kumwambia tarehe kama ile mwakani atakuwa na Nyumba yake.

Alisema kwa mshangao huku mamia ya watu walio hudhuria ibada hiyo wakishangilia Dada yule alisema kuwa lile neno limetimia kama mtumishi wa Mungu alivyosema na sasa anamiliki nyumba yake, japo zaidi ya miaka 10 hakufanikiwa kujenga.

Kwa upande wake Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Enlightened Christian Gathering Church Of Tanzania (ECG)Tawi la Kilimanjaro, Pastor Peter Ikera alisema kwa nanma ya pekee kabisa huyu Yesu, tunayemtumikia amefanya jambo kubwa, kwa nguvu ya Mungu aliye hai.

“Biblia inasema 'Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa', Huu ni wakati wa Yesu kutenda alisema Pastor Ikera.

Aidha  kumekuwa na  shuhuda mbalimbali kanisani hapo za watu waliofunguliwa na kuponywa magonjwa sugu, kama vile  kansa, uvimbe , kupooza, HIV, matasa kupata watoto, watu  kupata kazi na   kuinuliwa kwa kibali kisicho cha kawaida.

Upekee mkubwa wa mtumishi huyu wa Mungu ni uwezo wake na neema iliyo juu yake kuweza kuandaa makongamano makubwa mjini hapa ambayo hupelekea maisha ya watu wengi kufunguliwa na mamia kwa maelfu ya watu kumrudia kristo.

Makongamano haya ni pamoja na tukio la kihistoria la kumleta na kuandaa mkutano mkubwa ulio kusanya watu kutoma nchi nzima, na Africa Mashariki kwa ujumla mkutano ulio kuwa na watu takribani elfu ishirini ukihudumiwa na mtumishi wa Mungu muhubili wa Kimataifa Nabii Shepherd Bushiri kutoka Afrika ya kusini baba yake wa kiroho.
STORY by: Kija Elias
PHOTOS by: ECG
EDITED by: Jabir Johnson

Post a Comment

Previous Post Next Post