Kukiwa tulivu ndani
ya kanisa la Tanzania Assemblies of God Ilomba Jijini Mbeya majira ya saa 3:00
asubuhi ya Jumapili ya Februari 5 Mtumishi wa Bwana Mchungaji na Mwalimu Vinac
Amnon Mwakitalu anasimama na kuitaka hadhira ya waamini wa Kanisa hilo kutambua
kuwa Yesu anamtafuta mtu anayemtafuta.
MCHUNGAJI VINAC AMNON MWAKITALU
Akizungumza kwa msisitizo katika ibada hiyo ya kwanza
Mchungaji Mwakitalu alisema Yesu anakuwa rafiki wa Zakayo kwasababu Zakayo
alidiriki kumtafuta Yesu.
Katika mahubiri yake yaliyokuwa na kichwa kisemacho “KUOKOKA
NI KUBADILIKA” alinukuru maandiko kwenye Biblia Takatifu Luka 19:1-10 na kusema
Zakayo hakuwa rafiki wa jamii aliyokuwa nayo kutokana na sifa ya watoza ushuru.
Mchungaji Mwakitalu aliongeza kusema watoza ushuru walichukiwa na jamii
kutokana na tabia yao ya wezi, wakatili, waasherati, wenye kujipendekeza kwa
watawala hivyo Zakayo mpaka anamtafuta Yesu alikuwa katika uhitaji na nafsi
yake.
Pia Mchungaji Mwakitalu alisema kuokoka ni kubadilika ndani
ya Kristo na kuwataka wajichunguze kama wanabadiliko ndani ya Kristo na kwamba
hali zote mbaya mtu akishaokoka huondoka.
Aidha Mchungaji Mwakitalu alisema mabadiliko ya mwamini huja
kwa kusoma na kujifunza Neno la Mungu na kufanya maombi.
CHANZO: JAIZMELALEO