Wito
umetolewa kwa wanandoa kudumisha upendo kwa kuishi katika maisha ya ndoa yanayo
mpendeza mwenyezi Mungu ikiwa ni pamoja na kusaidiana katika shida na raha.
Mchungaji
wa kanisa la Pentecostal Evangelistic Fellowship Of Africa (PEFA) la Jijini
Arusha Noel Urio, ameyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati alipokuwa akifungisha
ndoa ya wawili hao kati ya Godlove na Florah, iliyofanyika katika kanisa la
PEFA la Mlimani Jijini Arusha..
Askofu mkuu wa kanisa la Furaha Tanzania Jones Molla (wa pili kutoka kulia), katika picha ya pamoja na wanandoa hivi karibuni jijini Arusha. |
Mchg
Urio, alisema ndoa ni muunganiko kati ya Mwanamme na mwanamke, na kuwaacha
wazazi wao na kuambatana na kuwa mwili mmoja , hivyo amewataka wanandoa hao kwenda kudumisha
upendo ndani ya ndoa yao.
Alisema
wazazi walio wengi wamekuwa chanzo kikubwa cha kusababisha ndoa za vijana wao,
kuvunjika pindi matatizo yanapotokea kati ya Baba na Mama, hivyo migogoro
inapozidi wanandoa hao waliokuwa wakipendana kabla ya kuoana huamua kuachana.
Aidha
Mchg Urio alisema, vijana wengi wamekuwa wakidondoka katika mtego wa
mwovu, kwa kuwa wamejikuta wakipendana
bila ya kumshirikisha Mungu katika kuanza mahudiano yao ya uchumba.
Alisema
jambo la msingi katika ndoa, hata kama usipokubali jambo hilo, imani hupuuzwa
na vijana wengi na ndio maana wengi waliopuuza wamekuwa wakijikuta wakilia na
ndoa zao.
“Kimsingi
Mungu hakukusudii kuona ndoa zikivunjike na kuvunjika kwa ndoa siku zote si
kitu chema machoni pa muumba ambaye ndiye mwanzilishi,”alisema Mchungaji Urio.
Aliongeza
kuwa “Nataka kuwaambia nyinyi Godlove na Florah, ndoa ya Kikristo huwa
haivunjiki kuoa sio sababu ya kuwa sahau wazazi wenu, waone ni nyumba ya
Baraka, wazazi wanahitaji heshima tu kwenu,”alisema
Hata
hivyo Mchg Urio, aliwataka wazazi kutokuingilia mahusiano ya watoto wao, kwani
kwa kufanya hivyo ni hatari kubwa, hivyo wazazi hawaruhusiwa kusababisha ndoa
za watoto wao kuvunjika.
Kwa
upande wake Askofu mkuu wa kanisa la Furaha Tanzania Jones Molla, ambaye kijana
wake Godlove ameona, aliwataka wawili hao kwenda kuishi maisha ya upendo.
“Katika
mfumo wa maisha aliyoweka Mwenyezi
Mungu, moja wapo ni Upendo wa kimwili
katika yam me na mke, kuishi pamoja
katika maisha ya ndoa,”alisema Askofu Molla.
STORY BY: Kija Elias
STORY BY: Kija Elias
0 Comments