Mwimbaji nyimbo za Injili Onesmus atua Kilimanjaro

Armstrong Kalua maarufu Onesmus
Mwimbaji wa Nyimbo za Injili kutoka Afrika Kusini mwenye makazi yake nchini Malawi Armstrong Kalua maarufu Onesmus ametua mjini Moshi mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya semina kwa njia ya nyimbo.

Chanzo kimoja kilisema mwimbaji huyo atafanya huduma hiyo mjini Moshi kuanzia Machi 29 hadi 31. Mbali ya kufanya huduma hiyo ya Neno la Mungu kwa njia ya Nyimbo atazindua albamu yake ya ‘Messenger’.

Mchungaji Peter Ikera ndiye mwenyeji wa mwimbaji huyo. Semina hiyo itafanyika katika Kanisa la ECG, Rau mjini Moshi.



Post a Comment

Previous Post Next Post