1. Umewahi kukutana na mtoto anayependa baba amtumie
"pocket money" lakini kimsingi hampendi baba yake? Umewahi kufikiri
siku baba yake akimwambia sina hela itakuwaje?
2. Umewahi kukutana na waziri mchapa kazi, mwenye ustadi wa
hali ya juu, anayependwa na watu kiasi kwamba wako tayari walale chini yeye
apite awakanyage juu, na kwasababu hiyo kawafanya watu hao hao wasiwe na mpango
na Rais aliyempa mamlaka akiwaaminisha watu yeye ndio jibu lao? Umewahi
kufikiri maumivu ya Rais aliyonayo?
3. Hivi umewahi kujiuliza kati ya glass na maji kipi ni
muhimu zaidi?
Hizi ni Kansa Hatari Sana kwa kanisa la leo...
1. Kupenda baraka kuliko kumpenda mtoa baraka
2. Kumtukuza mtumishi kuliko kumtukuza Mungu
3. Kuliinua na kuliheshimisha kanisa (mahali pa kuabudia)
kuliko kumuinua na kumheshimisha Mungu
NB: Pamoja na kwamba tuliambiwa tuwe na imani, lakini
hatukuambiwa tuziweke akili pembeni
Mtoaji wa Neno la Hekima: Paul Francis Masele
Tags
THEOLOJIA