HUDUMA ya kutafsiri Biblia na kuendeleza lugha asili katika mkoa wa Mbeya na Iringa (MCIP) inatarajia kukamilisha kutafsiri Injili ya Marko kwa lugha ya Kibena ifikapo Machi mwakani.
Wakizungumza katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hizi walisema kuwa kutafsiri Neno la Mungu kwa lugha za asil.i ni katika kutekeleza sera ya Taifa ya kutunza lugha za asili.Walisema lugha za jamii ni hazina ya historia, mila na desturi, teknolojia na utamaduni kwani ndio msingi mkuu wa lugha ya Kiswahili.
Pia walisema kuwa watu wanaoweza kusoma na kuandika Kiswahili wanaweza kujifunza kwa urahisi kusoma na kuandika lugha zao za asili na wasioweza kufaanya hivyo wakijifunza wataweza. Hata hivyo walisema kuwa wanaisaidia jamii na makanisa kukusanya na kuratibu nguvu zao hivyo kuongeza ufanisi.MCIP hadi sasa inashughulika na lugha 10 za mikoa ya Iringa ambazo ni Kibena, Kibungu, Kikinga, Kimalila, Kindal, Kinyakyusa, Kinyiha, Kisafwa , Kisangu na Kivwanji.