Blogu hii ilianzishwa mwaka Desemba 2009 na vijana watatu waliokuwa wakisali katika Kanisa la Tanzania Assemblies of God Msewe jijini Dar es Salaam. Vijana hao wa Idara ya Vijana (CA's) kanisa hapo waliona kuna ulazima wa kuendana na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA). Jabir, Hobokela na Fadhili walianza wakiwa na madhumuni ya kuufikia ulimwengu kwa kuandika taarifa mbalimbali na masomo yanahusu Ukristo.
Ukitaka mtu akujue unaweza kufanya nini? Utamwambia jina lako, sivyo? Je, Mungu ana jina? Dini nyingi hujibu kwamba jina lake ni Mungu au Bwana. Lakini hayo sio majina yake binafsi. Hayo ni majina ya heshima kama vile Mfalme au Rais. Biblia inafundisha kwamba Mungu ana majina mengi ya heshima. Baadhi ya majina hayo ni Mungu na Bwana. Hata hivyo Biblia inatufundisha pia kwamba Mungu ana jina lake binafsi, yaani YEHOVA.
0 Comments