WAKRISTO nchini Tanzania wametakiwa kujua kuwa utoaji ni tendo la Ibada kama yalivyo mambo mengine ndani ya wokovu.
Akihubiri katika Ibada Jumapili ya leo Mchungaji na Mwalimu Vinac Amnon Mwakitalu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Ilomba jijini Mbeya amesema wakristo walio wengi wa kizazi cha leo wanafikiri kutoa ni kwa manufaa ya watumishi wa Mungu pekee hali ambayo imefanya kutokuwa watoaji.
Pia amesema Kitabu cha Mambo ya Walawi kila Muisraeli alishiriki kumtolea Mungu kwani lilikuwa ni tendo la Ibada na lilikuwa na umuhimu sana katika maisha yao katika kudumisha ushirika na Mungu.
Hata hivyo amesema mwamini asipopenda kutoa mbele ni kujikwamisha katika maisha yake ya kila siku hasa ukizingatia ulimwengu kwa sasa umeshikwa kwa ubinafsi hali ambayo inasababisha hali ya maisha kupanda.
Aidha amewataka Wakristo kuchukua tahadhari kama kuachana na uchoyo na ubinafsi kama ambavyo ulimwengu na kujifunza kuwa mtoaji.