Askofu Evaristo Chengula wa Jimbo Katoliki la Mbeya, amemshauri Mheshimiwa Anna Makinda, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa mkakamavu zaidi katika maamuzi yake, wakati wa kuendesha shughuli za Bunge; akizingatia misingi ya haki, amani, usawa, bila kuteteleka kwa masilahi ya watanzania, kama njia ya kumkomboa na kumwendeleza mtanzania katika medani mbali mbali za maisha.
Askofu Chengula aliyasema hayo jijini Mbeya wakati Mheshimiwa Anna Makinda alipomtembelea Askofu Chengula, kwenye Makao yake Makuu, Kanisa kuu la Mtakatifu Antoni wa Padua, Mbeya mjini, mara baada ya kushiriki katika Ibada ya Misa Takatifu, Parokiani hapo.
Askofu Chengula alimpongeza Spika Anna Makinda kwa kuchaguliwa kushika wadhifa mkubwa kati ya mihimili mitatu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa ni mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuliongoza Bunge la Tanzania tangu ilipojipatia uhuru wake, yapata miaka arobaini na tisa iliyopita.
Alimshauri aendelee kuwa ni mchamungu, kwa kutegemea zaidi na zaidi maongozi yake, akijichotea hekima na busara ya kuliongoza Bunge katika vikwao vyake. Jimbo Katoliki la Mbeya, limesema, litaendelea kuwaombea viongozi wa Serikali ili waweze kutekeleza wajibu wao kwa ajili ya mafao ya wengi nchini Tanzania.
Askofu Chengula aliwashauri pia viongozi wa Serikali na vyama vya kisiasa kujenga uhusiano wa karibu na viongozi wa kidini, ili kubadilishana mawazo, mang'amuzi na uzoefu wao katika kuwahudumia watanzania katika medani mbali mbali za maisha.
Kwa upande wake, Spika Anna Makinda akizungumza na waumini wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Antoni wa Padua mara baada ya maadhimisho ya Fumbo la Ekaristi Takatifu, aliwataka kuendelea kuwa ni wachamungu zaidi ili kutomfungulia shetani milango na hatimaye, kuvuruga amani, upendo na mshikamano wa kitaifa ambao umedumu nchini Tanzania kwa miaka mingi sasa. Anasema, mustakhbali wa Tanzania uko mikononi mwa watanzania wenyewe.
Imeandikwa na Michael Mbighi
Imehaririwa na Johnson Jabir