MCHUNGAJI AWATAKA WAUMINI KUOMBA KWA ROHO..


WAKRISTO hapa nchini wametakiwa kuomba katika Roho Mtakatifu ili waweze kukua kiroho.
Akihubiri katika ibada Mchungaji Joseph Mnyawami wa Kanisa la Jesus Making Centre lililopo Sido Jijini Mbeya amesema wakristo wengi hawakui kiroho kwasababu katika maombi yao huomba kwa akili mno kuliko rohoni kama Biblia isemavyo. Mchungaji Mnyawami amesema ahapingi kuomba kwa akili kwani Biblia imesisitiza pia kuomba kwa jinsi hiyo lakini kuomba kwa roho huijenga imani ya mwamini. Hata hivyo amesema kuomba kwa roho hufaa sana pindi mkristo anapopitia chanagamoto mbalimbali kwani Mungu atamwonyesha kitu halisi ukilinganisha na Yule aombaye katika akili za kibinadamu. Aidha Mchungaji Mnyawami amesema Kanisa linatumbukia katika mambo ya ovyo kwa kuwa wakristo wengi huona wanaweza kufanya kwa akili zao.

Post a Comment

Previous Post Next Post