MCHUNGAJI na Mwinjilisti Leonard Lwesya kutoka Zanzibar amewataka wakristo hapa nchini kuwa na wivu na kazi ya Mungu badala ya kubakia kupiga majungu mitaani.
Akihubiri katika kanisa la Tanzania Assemblies of God Ilomba Mbeya alisema kuwa wakristo wengi huwa hawashtuki pindi wanapoona kazi ya Mungu inashindwa kuendelea kutokana na vikwazo mbalimbali ambavyo huletwa na waamini wenyewe kwa kujibweteka na kusahau wajibu wao. Mchungaji huo aliwakumbusha kuwa Eliya alikuwa na wivu na kazi ya Mungu na ndio maana hakupenda Mungu atukanwe hivyo alisimamia viwango vinavyotakiwa hata manabii 450 wa Baali walisalimu amri kwa Eliya. Hata hivyo aliwataka kuomba kwa bidii kwani haiwezekani bila kuliita Jina la Yesu pekee lenye uwezo wa kutenda mambo makubwa.