WATOTO WATAKIWA KUMTOLEA MUNGU


WATOTO wakristo wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God wametakiwa kuishi maisha ya kumtolea Mungu kama ambavyo Biblia inasisitiza kufanya hivyo.
Katika darasa la watoto hao Mwalimu Rachel Kitururu alisema watoto wa waamini wanatakiwa kuishi maisha ya kumtolea Mungu  kwani ni chanzo cha baraka kimwili na kiroho. Kwa upande wa Mwalimu Leokadia Katitu aliwaelekeza watoto hao kuwa fungu la kumi ni kutoa silimia kumi ya vitu katika mapato ayapatayo.
Katika darasa hilo watoto wapatao 71 walijifunza kwa kutumia kitabu cha Malaki sura ya 3:10 na Marko sura ya 12:41-44

Post a Comment

Previous Post Next Post