VIJANA WATAKIWA KUWA WAOMBAJI


MWENYEKITI wa Idara ya Mabalozi wa Kristo Daniel Lwesya wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God  Ilomba Mbeya amewataka vijana wa kanisa hilo kufanya maombi ya nguvu kwani ni agizo la Mungu.
Akifundisha somo katika mafundisho maalumu ya Jumapili kanisani hapo Lwesya alisema vijana wanatakiwa wajue Mungu anasikia maombi, wakati mara nyingi hawajibiwi kwasababu ya Maisha ya dhambi.
Hata hivyo aliongeza kusema wengine hufanya maombi ili kupata vitu ambavyo watavitumia kwa tama zao hali ambayo husababisha maombi yao kuchelewa kujibiwa. Na wakati mwingine Mungu huchelewa kwa sababu zake mwenyewe kwani sio kila uombapo lazima ujibiwe.
 Aidha alitoa wito kwa vijana hao kufanya maombi bila kukata tama kwani kwa kufanya hivyo kazi ya Mungu itasonga mbele. 

Post a Comment

0 Comments