WAKRISTO wametakiwa kuwa makini na imani potofu kufuatia wengi kuwa na sintofahamu na imani hizo.
Akifundisha katika darasa la Waamini wapya Mzee Patrick Nkwama alisema imani hizo huja kwa sura ya Kimungu huku ndani yake zikiwa na sura ya shetani.
Mzee Nkwama aliongeza kusema kuwa imani hizi huja na ufumbuzi wa matatizo ya mwanadamu na kwa uchache sana kufundisha kutubu na kumwelekea Mungu..
Hata hivyo aliwataka wakristo hao kujifunza kwa bidii Neno la Mungu ili kuzijua kwani katika kusoma Neno la Mungu Roho Mtakatifu atamfunulia zaidi ya hapo.
Wakati huo huo wakristo wa Kanisa hilo wametakiwa kuwa na ushirikiano uliotajwa katika Biblia ili kukuza mshikamano na upendo.
Hayo yalijiri katika Shule ya Uanafunzi katika somo la saba lilikuwa na kichwa kisemacho “UMOJA KATIKA KANISA” kufuatia nguvu za Mungu kwa kanisa la sasa kupungua kutokana na kuwa kusaidiana katika mambo mbalimbali kutoweka na somo hilo lilifundishwa na Mwalimu Michael Mwashilindi.