Uvumilivu, kukaa kimya wakati wa changamoto za
maisha, kuheshimu uongozi uliopo na kujua kuwa ahadi za Mungu kwa mtu wake
zitatimilika kwa wakati wake ni mambo ya msingi katika maisha ya Mkristo.
MCHUNGAJI VINAC AMNON MWAKITALU
Akihubiri katika Ibada ya Jumapili
Mchungaji na Mwalimu Vinac Amnon Mwakitalu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of
God Ilomba Mbeya alisema hizo zilikuwa kanuni za msingi katika maisha ya Mfalme
Daudi kabla ya kukalia kiti hicho na hata baada ya kuingia madarakani.
Mchungaji Mwakitalu
alisema mwamini anapaswa kuwa mvumulivu na mwenye subira pindi apitiapo
changamoto mbalimbali za kimaisha kubwa zaidi kukaa kimya na kumsubiri Mungu
atende kwa wakati wake.
Aliongeza kusema wakristo
wamefikia hatua mbaya pindi waingiapo kwenye changamoto za kimasiha kujikuta
wakimwacha Mungu huku wakiendelea kuingia katika majumba ya Ibada hali ambayo
ameiita kuwa ni kupoteza muda.
Mchungaji Mwakitalu
aliongeza kusema Daudi alipotenda dhambi alitubu mara moja kwani ndani yake
alikuwa na Roho wa Mungu, na kwamba hata siku za leo kwa mtu aliyejaa Roho
Mtakatifu hawezi kukaa kimya akisha
tenda dhambi.
Hata hivyo Mchungaji
Mwakitalu aliwataka waumini wa kanisa hilo
kwa ujumla wake kuwa waombaji ili kuendelea kutunza ushirika na Mungu na kuwa
wa kipekee katika jamii.
Aidha Mchungaji Mwakitalu
aliweka bayana maisha ya Daudi ya kujali Ibada na kazi ya Mungu kwa ujumla.
Johnson Jabir
Januari 23, 2012