WATUMISHI WA MUNGU WANAPOSAHAU KUWAFUNDISHA WAUMINI MAISHA YA UTAKATIFU KATIKA UKRISTO.

Biblia ni kitabu chenye mfanano na upekee kama vitabu vingine hapa ulimwenguni.
 Tunaposema BIBLIA ina mfanano na vitabu vingine ina maana ya kuwa imezingatia uandishi wa lugha husika, uchapishaji na mengine mengi ya kitaaluma.


Upekee wa BIBLIA unakuja pale tu yaliyoandikwa humo ya uvuvio wa Mungu Mwenyezi aliyezifanya mbingu na nchi kwa maana nzuri si kwa makusudi ya wanadamu bali kwa uweza wa Aliye juu ya yote.
Biblia maana yake ni mkusanyiko wa vitabu na kuunganishwa pamoja vyenye kuleta maana. Na Neno hili lilitoka kwa Wayunani “Biblos”


Wakristo kwaujumla wake licha ya kupishana sana katika baadhi ya misimamo kuhusu Mungu lakini wote hutumia kitabu hiki chenye mkusanyo wa vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi mbalimbali waliovuviwa na Mungu.


Imegawanywa  katika sehemu mbili ambazo ni Agano la Kale na Agano Jipya
Vitabu hivyo ni
Agano la Kale
1
Mwanzo
Mwa.
2
Kutoka
Kut.
3
Mambo ya Walawi
Law.
4
Hesabu
Hes.
5
Kumbukumbu la Torati
Kumb.
6
Yoshua
Yos.
7
Waamuzi
Amu.
8
Ruthu
Rut.
9
1 Samweli
1 Sam.
10
2 Samweli
2 Sam.
11
1 Wafalme
1 Fal.
12
2 Wafalme
2 Fal.
13
1 Mambo ya Nyakati
1 Nyak.
14
2 Mambo ya Nyakati
2 Nyak.
15
Ezra
Ezr.
16
Nehemia
Neh.
17
Esta
Est.
18
Ayubu
Ayu.
19
Zaburi
Zab.
20
Mithali
Mith.
21
Mhubiri
Mhu.
22
Wimbo ulio Bora
Wim.
23
Isaya
Isa.
24
Yeremia
Yer.
25
Maombolezo
Omb.
26
Ezekieli
Eze.
27
Danieli
Dan.
28
Hosea
Hos.
29
Yoeli
Yoe.
30
Amosi
Amo.
31
Obadia
Oba.
32
Yona
Yon.
33
Mika
Mik.
34
Nahumu
Nah.
35
Habakuki
Hab.
36
Sefania
Sef.
37
Hagai
Hag.
38
Zekaria
Zek.
39
Malaki
Mal.
Agano Jipya
1
Mathayo
Mt.
2
Marko
Mk.
3
Luka
Lk.
4
Yohana
Yn.
5
Matendo ya Mitume
Mdo.
6
Warumi
Rum.
7
1 Wakorintho
1 Kor.
8
2 Wakorintho
2 Kor.
9
Wagalatia
Gal.
10
Waefeso
Efe.
11
Wafilipi
Flp.
12
Wakolosai
Kol.
13
1 Wathesalonike
1 The.
14
2 Wathesalonike
2 The.
15
1 Timotheo
1 Tim.
16
2 Timotheo
2 Tim.
17
Tito
Tit.
18
Filemoni
Flm.
19
Waebrania
Ebr.
20
Yakobo
Yak.
21
1 Petro
1 Pet.
22
2 Petro
2 Pet.
23
1 Yohana
1 Yn.
24
2 Yohana
2 Yn.
25
3 Yohana
3 Yn.
26
Yuda
Yud.
27
Ufunuo
Ufu.



Katika Mahojiano maalum na Askofu Mbetwa wa Kanisa la Philadephia  lililopo Mabatini Jijini Mbeya anweka mkazo zaidi katika ari ya watumishi wa Mungu kushindwa kuwafundisha waumini wao maisha ya kila siku na mustakabali wao baada ya maisha ya hapa duniani 
 ASKOFU MBETWA " Mzee wa Maboresho"

Mahojiano hayo yalikuwa hivi:


MCRCTV: Unazungumziaje hali ya Utakatifu kwa sasa katika Kanisa la Mungu?
ASKOFU MBETWA: Unapozungumizia utakatifu au kwa lugha rahisi twaweza kusema maisha safi mbele za Mungu katika kanisa hayako katika hali ambayo Mungu anataka. 


MCRCTV: Nani alaumiwe kuhusu hilo kwa sasa ni ninyi watumishi wa Mungu au waumini wenu?
ASKOFU MBETWA: Hapa wa kulaumiwa ni kiongozi wa kanisa husika kwani amewekwa na Mungu ili aongoze watu katika njia iliyo sahihi , nah ii inatokana na watumishi wa Mungu kutokuwa na wito.


MCRCTV: Unaposema wito haumo ndani viongozi hao wa makanisa una maana gani?
ASKOFU MBETWA: unajua kuna aina tatu za watumishi wa Mungu, Mosi Aliyeitwa (Mwenye wito), Pili Aliyetaka na Tatu, Aliyepewa.


MCRCTV: Unaweza kuweka bayana undani wa aina hizo za watumishi wa Mungu uliowataja?
ASKOFU MBETWA: Nikianza na Aliyeitwa ni kwamba Mungu anakuwa ameweka moja kwa moja kitu ndani yake kwa ajili ya watu wa Mungu pasipo kujali mazingira yanayomzunguka na Roho wa Mungu ndio njia yake  na dira yake kuu katika huduma ya kulichunga kanisa la Mungu na mara nyingi utagundua mabadiliko katika maisha ya waumini huonekana sio katika mwili tu, pia katika nafsi zao na roho zao kuhusu Mungu.
Mtumishi wa Mungu aliyetaka ni kwamba mazingira yanamhamasisha kutaka kazi au huduma ya kulichunga kanisa la Mungu; huenda ameona hana la kufanya hivyo  huamua kusomea kazi ya kuliongoza kanisa la Mungu na hatimaye kusimikwa.
Mtumishi wa Mungu aliyepewa ni yule ambaye anashawishiwa na watu kuwa angefaa kukaa na kulichunga kanisa la Mungu, hivyo anaweza kushawishiwa na waumini wenzake, maaskofu na watumishi wengine kuwa aende kusomea huduma hiyo na akishahitimu hupewa kanisa.


MCRCTV: Nini changamoto za Watumishi wa Mungu hao uliowataja?
ASKOFU MBETWA: Changamoto yao ni kwamba aina ya watumishi wa Mungu waliotaka wenyewe na kupewa hujikuta wakiingia katika malumbano kuhusu watumishi wa Mungu walioitwa na kuonekana wale wenye wito wanajidai hivyo badala ya kukaza kufundisha maisha ya kila siku ya mwamini na kwa namna gani aenende huanza kupoteza mwelekeo na dhambi huingia kanisani na kuchafua kabisa hali ya hewa mbele za Mungu.


MCRCTV: Nini wito wako kwa watumishi wenzako wa Mungu na Kanisa kwa ujumla?
ASKOFU MBETWA: Ningependa kusisitiza kwamba Nyaraka za Mtume Paulo zinaelekeza zaidi maisha ya kila siku ya mwamini katika Kristo ni vema wakristo wote wakiwemo na viongozi wao kupenda kusoma na kutendea kazi ili kuendelea kumtuinza Roho Mtakatifu.
Johnson Jabir
Januari 21, 2012

Post a Comment

0 Comments