YAH: KUDHALILISHWA KWA RAIS
KIKWETE KWENYE FACEBOOK
Blogu ya JAIZMELALEO
ikishirikiana na blogu ya MCRCTV kwa pamoja tunapenda kutoa msimamo wetu katika
suala hili la matumizi ya mtandao.
Katika
ukurasa wa facebook kuna picha mabayo si haki na ni kitendo cha aibu kwa Mkuu wa
nchi ya Tanzania Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete kuonyeshwa katika vazi la
kikahaba.
Yapo
matukio mengi ya viongozi wengi ulimwenguni wanaofanyiwa hivyo lakini kwa kuona
umuhimu kwa taifa na watumiaji wa mitandao ya kijami kilichofanyika hapo sio
haki hata kama ni uhuru basi umepitiliza.
Anuani
hiyo imeandikwa “FISADI KIKWETE” kutoka Dar es Salaam Tanzania ambayo katika
profile picture imewekwa picha hiyo bofya linki hii.
TUNASEMA
hii ni kashfa hatua za makusudi lazima zichukuliwe kwa mtu au kundi la watu
wanaojihusisha na tabia hizi za udhalilishaji kwa kiongozi mkubwa kama huyu
mwenye heshima nchini Tanzania.
Licha
ya kwamba kwa upande wake kama Rais anatakiwa aichukue kama changamoto ili kujipanga
vizuri, kujichunguza nyendo zake bila hivyo zitazidi zaidi ya hapo.
TUNAWAOMBA
watanzania waheshimu maadili ya mtanzania hata kama kuna makosa kwa mtu husika
lakini taratibu zipo na zichukuliwe.
UONGOZI
WA BLOGU ZA JAIZMELALEO NA MCRCTV
Januari
20, 2012