U
|
ongozi wa Ushirika wa Kikristo wa Wanavyuo Tanzania(USCF) mkoa wa Mbeya unatarajia kufanya
Kongamano la Pasaka litakalofanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu Huria Tanzania
Kampasi ya Mbeya.
Mwenyekiti wa USCF Mbeya Peniel Sarakikya
amesema Kongamano hilo
lenye Kauli Mbiu KUENENDA KATIKA ROHO
litaanza Aprili 6 hadi 8 mwaka huu.
Sarakikya ameongeza kusema kiingilio
kitakuwa Shilingi 10,000/= za Tanzania
ambapo ndani yake kwa wale waliotoa watakuwa wakipata chakula cha mchana.
Pia Mwenyekiti huyo amewataja watumishi wa
Bwana watakao fundisha katika Kongamano hilo ni Mchungaji Nguvila, Mchungaji
Oscar, Mchungaji Prince Mollel, Mchungaji Mariam Kyomo, Mchungaji Erick,
Mwalimu George Makoja na Mtume Paul
Njoroge.
CHANZO: USCF Mbeya