WANAFUNZI wa Vyuo Vikuu mkoani Mbeya wametakiwa kulishika Neno la Mungu
ili wamuone Mungu katika maisha yao
wawapo masomo.
Akifundisha katika Kongamano la
Pasaka kwa wanafunzi hao lililofanyika katika katika ukumbi wa Mbeya Sekondari
Jijini Mbeya; Mwalimu George Makoja alisema Shetani amekuwa mjanja sana tangu kuumbwa kwa ulimwengu ili
kumrudisha mwanadamu nyuma asijua uzuri wa Mungu Mwenyezi.
Mwalimu George alisema kuwa Neno
la Mungu ni chanzo cha mafanikio ya kiroho, kimwili hata nafsi hivyo kulishika
kwa umakini mkubwa ni jambo la muhimu sana.
Hata hivyo alinukuru maandiko kutoka
Biblia kwenye vitabu vifuatavyo kutioa uzito; Luka 4:1-; Yoshua 1;8.
Aidha alisema kuwa katika vyuo
vikuu kumwemwagwa mapepo kwa ajili ya
kuteketeza kundi hili la vijana na kwamba ili kujilinda Neno ala Mungu ndilo
Jibu.
Walimu katika Kongamano hilo la USCF walikuwa Mchungaji Nguvila, Mchungaji
Oscar, Mchungaji Prince Mollel, Mchungaji Mariam Kyomo, Mchungaji Erick,
Mwalimu George Makoja na Mtume Paul
Njoroge.
Kongamano la USCF limehitimisha jana Aprili 8, 2012.