“
|
MAISHA YALIYO NA NIDHAMU HUWA YA FURAHA NA HEKIMA” ndivyo ambavyo
Mwalimu wa Shule ya Uanafunzi wa Darasa la Mabalozi wa Yesu (C.A’s) wa Kanisa
la Tanzania
Assemblies of God Ilomba Mbeya alivyaoanza kufundisha.
Akifundisha kwa msisitizo Mwalimu Maria
Nkwama aliwaasa wanafunzi hao kulishika Neno la Mungu kwani sio kwa faida ya sasa
pekee bali hata kwa vizazi vijavyo.
Pia aliongeza kuwa hakuna mtu kwa asili
ambaye alizaliwa akiwa na tabia njema hivyo kumfanya awe mzuri ni lazima atengenezwe kwa mafundisho ya Neno la Mungu.