Watu wasiojulikana jana wamempiga risasi Father, Ambros
Mkenda wa Kanisa Katoliki la Mpendae Mjini Zanzibar nje ya nyumba yake majira
ya saa 12 jioni wakati akitokea kanisani.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini
Magharibi Aziz Juma Mohammed amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo
alisema Father amepigwa risasi na ameumizwa sehemu ya kichwa na amekuwa akitoka
damu nyingi kichwani na tayari anapatiwa matibabu katika hospitali kuu ya Mnazi
Mmoja.
ZAIDI BOFYA : JAIZMELALEO