LEO
NI CHRISMAS
Krismasi (pia Noeli)
ni sikukuu
ambako Wakristo husheherekea kuzaliwa kwake Yesu Kristo
zaidi ya miaka 2000 iliyopita. Kwa kawaida husheherekewa tarehe 25 Desemba
katika Ukristo
wa magharibi na tarehe 6 Januari katika ule wa mashariki.
Historia ya Krismasi
Tarehe halisi ya kuzaliwa kwake Yesu haijulikani kwa
sababu utamaduni
wa Wayahudi
wa wakati ule haukuwa na sherehe au kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa.
Lakini
baadaye Ukristo
ulienea katika Dola la Roma na kati ya mataifa yaliyokuwa na kawaida
ya kuzingatia siku ya kuzaliwa. Hivyo ilijitokeza hamu ya kusheherekea pia
sikukuu ya kuzaliwa kwake Kristo. Ndiyo asili ya Sikukuu ya Krismasi.
Tangu
mwanzo wa karne
ya 3 BK kuna kumbukumbu ya waandishi mbalimbali waliojadili tarehe ya
kuzaliwa kwake Yesu Kristo.
Habari
za kwanza kabisa za makadirio ya tarehe ya kuzaliwa kwake Yesu zinapatikana
kutoka Misri mnamo
mwaka 200. Mwandishi
Mkristo Klemens wa Alexandria (kitabu cha
Stromateis I, xxi) alilalamikia udadisi wa wataalamu kadhaa wa Misri
waliodai kwamba wamekadiria tarehe hiyo katika mwezi Mei, wengine katika Aprili. Alisema pia
kuwa kikundi cha Kikristo cha wafuasi wa Basilides huko Misri walisheherekea Epifania pamoja
na kuzaliwa kwake Yesu tarehe 6 Januari.
Labda
kadirio la tarehe ya Desemba 25 pia lina asili katika Misri. Kuanzia mwaka 200
(kwa mara ya kwanza katika maandishi ya Sixtus Julius Africanus)
tunasikia kwamba wataalamu wa Misri walifikiri tarehe 25 Machi
ilikuwa tarehe ya kufa kwake Kristo na pia siku ya kuzaliwa kwake. Kwa kuongeza
miezi tisa ya mimba inajitokeza 25 Desemba kama tarehe ya kuzaliwa.
Inaonekana
tarehe 25 Desemba ilijitokeza wakati huo. Kuna taarifa ya mwaka 204 kutoka Ipolito wa Roma kwamba tarehe 25
Desemba ilikuwa sikukuu ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo.
ZAIDI BOFYA LINKI HII