“Tasnia
ya Uimbaji hususani wa nyimbo za Injili hapa nchini kuna wakati inakwaza kweli
na kwa upande mwingine inabariki” …
Ndivyo alivyoanza kujieleza
Mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini Tanzania Esta Bukuku katika mahojiano na JAIZMELALEO siku chache zilizopita.
Esta Bukuku ambaye ni muumini
wa Madhehebu ya Kipentekoste ni mama wa watoto watatu ambao ni Eli, Kelvin na
Benjamin anafanya kazi zake nchini za kupeleka ujumbe wa Neno la Mungu kwa njia
ya Uimbaji uliotukuka.
Hadi hivi sasa ana Albamu moja
tu aliyoitoa mwaka 2011 “WATESI WANGU”
Alipoulizwa ni kwanini aliipa
jina hilo Mwanamke huyo mwenye Mume mmoja anayeitwa Jojo Sanga alisema kuna wakati alaipitia mapitoa amabayo
ahakuyataja isipokuwa alisema mambo amabayo yalimsononesha sana hata kufikia
wakati ambao alihisi kuna watu wanafurahi jinsi anayopitia masahibu hayo.
CHANGAMOTO
Esta
Bukuku anasema katika Muziki wa Injili una changamoto zake kwa sasa kutokana na
ukweli kwamba kuna waimbaji wengine wamekaa kibiashara zaidi hali ambayo
imeshusha sana kiwango cha kazi zao.
Pia anasema jamii imekuwa
ikiwaibia haki miliki. Hapa aligusia mkataba ambayo anaingia na msambazaji wa
kazi ya muziki kwamba wamekuwa wakiwaibia kutokana na kuendelea kutoa “copy”
zaidi bila ya faida kwa mwimbaji ambaye ndiye aliyetakiwa kufaidika.
WITO
Esta
Bukuku ametoa wito kwa jamii kuacha “ku-burn” kazi zao kwani kufanya hivyo ni
kosa kisheria.
CHANZO:
JAIZMELALEO