6 Julai 2014
Jumapili
Venue:
Amani Cathedral Centre
Soweto,
Moshi-Kilimanjaro.
Mhubiri:
Mama Mchungaji Benjamin Bukuku
Sura
Kuu: 1 Nyak. 28:9
Kichwa:
KUMJUA MUNGU
MAMA
MCHUNGAJI BENJAMIN BUKUKU
Katika
ibada hiyo iliyokuwa na watau zaidi ya 200, Mtumishi wa Bwana alianza kwa
kusema Kumjua Mungu, sio kazi nyepesi. Inahitaji muda wa kutosha nah ii ndio
sababu ya waumni kutakiwa kuwemo hekaluni mwa Bwana, kila kukuchapo.
Daudi aliona vema, kumrithisha
mtoto wake, Mungu aliyezifanya Mbingu na nchi. Daudi alijua wazi kwamba mali za dunia hii haziwezi kumsaidia
sana Suleiman bali kumfahamu Mungu ndio kila kitu.
Usipomjua
Mungu kiundani utateswa na kila uchafu wa dunia hii. Kumetokea imani nyingi
zinazodai kuwa zinamhuburi Mungu Aliye juu, lakini ukizichunguza sana utagundua
imani hizo hazina chochote zaidi ya kuwatesa binadamu.
Zab:23
1.
BWANA ndiye mchungaji wangu,
Sitapungukiwa na kitu….
Bwana Mungu anapaswa kuwa
mchungaji wa maisha yako siku zote za maisha yako hapa ulimwenguni.
1
Sam. 16:1-
Unamjua Mungu wako, ni wa namna
gani? Hapa kuna alama ya msingi…. “Naked eye” (macho ya nyama). Macho ya nyama
yanweza kukupa matokeo tofauti (wakati mwingine) sio mara zote yatatoa jawabu
sahihi.
Huwezi kumjua Mungu kirahisi,
kama husomi Neno lake kwani huko ndiko kwenye siri ya mafanikio.
1
Sam. 17:22-
Ukimtafuta , ataonekana bila
shaka. Ukimjua Mungu utafanya kazi yake kutokana na uwezo aliokupa. Tunaona
tena hapa “naked eye” inavyoweza kuleta matokeo mazuri ama mabaya.
Daudi+
Goliathi+
Majeshi
ya Israeli+
Majeshi
ya Wafilisti+
Majeshi ya Maadui yatakuja kwa
njia moja baada ya “timbwili” yatatoka nduki kwa njia saba. Katika safari ndefu
ya KUMJUA MUNGU kuna mengi yaumizayo lakini hupaswi KUKATA TAMAA.
Wafilipi
3:7
Inahitaji muda wa ziada katika
kuutafuta uso wake ili kufikia UKAMILIFU (dhambi haitapata nafasi)
Imba wimbo huu
“More
About Jesus R 432”
Nyimbo
za Injili Na. 59
“Nizidi
Yesu Kumjua”
Stanza
1.
Nizidi
Yesu kumjua,
Mapenzi
yake kufanya,
Na
nizidi kuzijua
Pendo
na wokovu pia
Chorus:
Zaidi
ya Yesu,
Zaidi
ya Yesu,
Nizidi
kumjua sana
Pendo
na wokovu pia.
Imetayarishwa
na Jabir Johnson, Septemba 7, 2014
Tags
TANZANIA