Sababu zilizowafanya Adam na Hawa wapoteze makao






Mwanzo 2:16, 17; 3:1-13, 24; Ufunuo 12:9; Tazama yaliyotendeka. Adamu na Hawa walifukuzwa katika bustani nzuri ya Edeni. 

Unaijua sababu? Walifanya jambo bay asana machoni pa Yehova. Yehova akawaadhibu. Unajua jambo baya ambalo Adamu na Hawa walifanya? Ni jambo ambalo Mungu aliwakataza. Mungu aliwaambia wale chakula chochote katika miti ya bustani. 

Lakini si cha mti ambao Mungu aliwakataza, ili wasife. Huo ulikuwa mti wake peke yake. Tunajua ni makosa kuchukua kitu cha mtu mwingine, sivyo? Basi kulitokea nini? Siku moja Hawa alikuwa peke yake katika bustani, nyoka alisema naye. 

Ajabu! Akamwambia hawa ale tunda la mti ambao Mungu aliwakataza. Yehova hakuumba nyoka waseme. Mtu fulani alifanya nyoka aseme. Ni nani huyo? Si Adamu. Ni mmoja wa watu ambao Yehova alikuwa ameumba zamani kabla ya dunia. Ni malaika ambao hatuwezi kuwaona. Malaika huyo mmoja akawa na kiburi sana. 

Alianza kuwaza kwamba ingefaa atawale kama Mungu. Alitaka watu wamtii yeye kuliko Yehova. Huyo ndiye malaika aliyemfanya nyoka aseme. Malaika huyo alimdanganya Hawa. Alipowaambia watafanana na Mungu wakila tunda hilo, Hawa aliamini. 

Hawa akala, pia akampa na mumewe Adamu. Adamu na Hawa hawakumtii Mungu. Ndiyo sababu walipoteza makao yao mazuri. Lakini siku moja Mungu ataifanya dunia nzima iwe nzuri kama bustani ya Edeni. Tutajifunza namna ya kuifanya hivyo. Lakini sasa tuchunguze yaliyowapata Adamu na Hawa.

Post a Comment

0 Comments