Zaburi 83: 18; Mwanzo 1:26-31; 2:7-25: Unaona tofauti gani katika uumbaji wa binadamu. Mwanamume na mwanamke wa kwanza. Nani aliwaumba? Ni Mungu. Unajua jina lake? Ni Yehova.
Mwanamume na mwanamke waliitwa Adamu na Hawa. Yehova Mungu aliumba Adamu hivi. Alichukua mavumbi akafanya mwili mzuri wa mwanamume. Kisha akapuliza katika pua, Adamu akawa hai. Yehova Mungu alimpa Adamu kazi ya kuwapa wanyama wote majina.
Labda Adamu aliwatazama wanyama muda mrefu ili aweze kuwachagulia majina bora. Adamu alipokuwa akiwa wanyama majina aliona jambo fulani. Unajua ni jambo gani?
Wanyama wote
walikuwa na wenzao. Tembo baba na mama walikuwapo, hata samba baba na mama
walikuwapo. Lakini Adamu hakuwa na mwenzake. Basi Yehova akampa Adamu usingizi mzito, akachukua ubavu
wake mmoja.
Kwa ubavu huo, Yehova alimfanyia Adamu mke. Adamu akafurahi! Wazia
Hawa alivyofurahi alipowekwa katika bustani hiyo nzuri! Wangeweza kuzaa watoto
wakae pamoja kwa furaha.
Yehova alitaka Adamu na Hawa wakae milele. Alitaka
waifanye dunia nzima iwe nzuri kama bustani hii ya Edeni. Adamu na Hawa
walifurahia sana hilo. Wewe ungependa kuifanya dunia iwe bustani nzuri?
Lakini
furaha ya Adamu na Hawa haikuendelea. Kwanini haikuendelea. Zaburi 83: 18; Mwanzo 1:26-31; 2:7-25:
Tags
THEOLOJIA